Lugha Nyingine
Xi Jinping akutana na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev mjini Shanghai

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev, ambaye yuko China kuhudhuria Mkutano wa AI Duniani 2026 na Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Usimamizi wa AI Duniani, mjini Shanghai, mashariki mwa China, Julai 16, 2026. (Xinhua/Zhai Jianlan)
SHANGHAI - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev, ambaye yuko China kuhudhuria Mkutano wa AI Duniani 2026 na Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Usimamizi wa AI Duniani huko Shanghai, mashariki mwa China jana Alhamisi.
Xi amesema kuwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote wa China na Kazakhstan umedumisha mwelekeo wa maendeleo yenye nguvu, ukionyesha uwezekano mkubwa kwa ushirikiano na matarajio mapana kwa maendeleo ya siku za baadaye.
Ametoa wito kwa pande hizo mbili kuimarisha hali ya kuhusiana na mikakati na sera za maendeleo na kuungana mkono ili kuinua ushirikiano wa kufuata hali halisi siku hadi siku.
Xi amesisitiza hitaji la kuboresha muundo wa biashara na kukuza aina mpya za shughuli katika biashara ya mtandaoni ya kuvuka mipaka na biashara za huduma. Pia ametoa wito wa kupanua ushirikiano katika rasilimali za nishati na madini na kuharakisha utekelezaji wa miradi muhimu.
Xi amehimiza juhudi za kusukuma mbele mafungamano ya mawasiliano kwa kupitia kuongeza usafiri wa ndege wa moja kwa moja na kuboresha usafirishaji kirahisi kwenye barabara za kimataifa. "China iko tayari wakati wote kuchangia teknolojia katika uchumi wa kidijitali na AI ili kuunga mkono mabadiliko ya muundo wa kidijitali ya Kazakhstan," Xi ameongeza.
Amesema China iko tayari kufanya ushirikiano na Kazakhstan katika kutekeleza mapendekezo manne kuhusu Dunia, na kuratibu na kushirikiana zaidi chini ya mifumo ya pande nyingi, ikiwemo Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai na mfumo wa China-Asia ya Kati, ili kulinda kwa pamoja usawa na haki kimataifa.
Kwa upande wake Tokayev amesema anafurahi sana kuja Shanghai, jiji lililojaa nguvu hai za uvumbuzi, na kuhudhuria Mkutano wa AI Duniani.
"Kazakhstan inauchukulia uhusiano wake na China kuwa jukumu la kwanza katika sera yake ya mambo ya nje," amesema Tokayev, akidhihirisha kuwa Kazakhstan inatarajia kudumisha mawasiliano ya karibu na China kwenye ngazi ya juu na kuimarisha ushirikiano wa kufuata hali halisi katika sekta za biashara, uwekezaji, mawasiliano na uchukuzi, nishati, kilimo na uchumi wa kidijitali.
Amesema Kazakhstan iko tayari kudumisha uratibu wa kiwango cha juu na China kwenye majukwaa ya pande nyingi na kufanya juhudi za kushirikiana katika kuhimiza usimamizi wa AI duniani.Baada ya mkutano huo, marais hao wawili walishuhudia utiaji saini wa mfululizo wa nyaraka za ushirikiano katika sekta za uchumi na biashara, mawasiliano na uchukuzi, mambo ya fedha na vyombo vya habari.

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev, ambaye yuko China kuhudhuria Mkutano wa AI Duniani 2026 na Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Usimamizi wa AI Duniani, mjini Shanghai, mashariki mwa China, Julai 16, 2026. (Xinhua/Zhai Jianlan)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



