Lugha Nyingine
Nchi 29 zasaini makubaliano ya kuanzisha Shirika la Ushirikiano wa AI Duniani

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akihudhuria hafla ya utiaji saini na kusaini makubaliano ya kuanzisha Shirika la Ushirikiano wa AI Duniani (WAICO) kwa niaba ya serikali ya China mjini Shanghai, mashariki mwa China, Julai 16, 2026. (Xinhua/Wang Ye)
SHANGHAI - Nchi ishirini na tisa zimesaini makubaliano mjini Shanghai jana Alhamisi juu ya kuanzisha Shirika la Ushirikiano wa AI Duniani (WAICO).
WAICO litakuwa shirika la kujitegemea la kiserikali la kimataifa lenye makao yake makuu mjini Shanghai, kwa mujibu wa makubaliano hayo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesaini makubaliano hayo kwa niaba ya serikali ya China.
Wajumbe kutoka nchi 29, zikiwemo Kazakhstan, Laos, Pakistan, Urusi na Indonesia, wamesaini makubaliano hayo, na kuzifanya nchi zao kuwa nchi wanachama waanzilishi wa WAICO. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ni miongoni mwa wajumbe kutoka nchi na mashirika ya kimataifa waliohudhuria hafla hiyo ya utiaji saini.
Shirika hilo litashikilia madhumuni ya Katiba ya Umoja wa Mataifa, kutekeleza dhana ya mashauriano ya kina na mchango wa pamoja kwa manufaa ya wotena kufuata mbinu inayotilia maanani zaidi watu, makubaliano hayo yanasema.
Linalenga kuhimiza ushirikiano wa kimataifa na usimamizi wa dunia juu ya AI, kuhakikisha kwamba AI inakuwa yenye manufaa, salama na ya haki, na hivyo kuhimiza maendeleo bora na yenye utaratibu ili kunufaisha binadamu wote.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akihudhuria hafla ya utiaji saini na kusaini makubaliano ya kuanzisha Shirika la Ushirikiano wa AI Duniani (WAICO) kwa niaba ya serikali ya China, sambamba na wajumbe wa nchi zingine mjini Shanghai, mashariki mwa China, Julai 16, 2026. (Xinhua/Wang Ye)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



