Lugha Nyingine
Xi atoa wito wa usimamizi AI duniani wenye usawa na kutangaza jumuiya mpya ya ushirikiano

Rais wa China Xi Jinping akitoa hotuba kuu kwenye hafla ya kufunguliwa kwa Mkutano wa AI Duniani 2026 na Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Usimamizi wa AI Duniani mjini Shanghai, mashariki mwa China, Julai 17, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)
SHANGHAI - Rais wa China Xi Jinping ametangaza kuanzishwa kwa Jumuiya ya Ushirikiano wa AI ya Dunia, na ametoa wito wa kufanya juhudi za pamoja za kujenga mfumo wa usimamizi wa AI duniani wenye haki na usawa.
"Nchi zote zinapaswa kuendeleza AI kwa njia ya kutoa kipaumbele kwa watu, na kusukuma mbele maendeleo ya AI kwa mwelekeo mzuri wa kuhimiza hamasa. Tunapaswa kuhakikisha teknolojia ya AI inaweza kuwa msukumo muhimu kwa kuchangia ustawi na usalama wa pamoja," Xi alisema Ijumaa iliyopita wakati akihutubia ufunguzi wa Mkutano wa AI Duniani 2026 (WAIC) na Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Usimamizi wa AI Duniani mjini Shanghai.

Picha hii iliyopigwa Julai 16, 2026 ikionyesha hali ya nje ya Kituo cha Maonyesho na Mikutano cha Maonyesho ya Dunia cha Shanghai China. (Xinhua/Ding Ting)
"Dunia imeingia katika kipindi ambacho hakijawahi kutokea cha uvumbuzi hai kwenye teknolojia za AI," Xi alisema kwenye hotuba yake kuu. Alitoa maswali kuhusu namna gani wanadamu wanaweza kupatana na mashine zinazoweza kufikiri, namna gani usalama unaweza kuhakikishwa wakati algoriti ikiwa sehemu ya kufanya maamuzi, namna gani watu wanaweza kukabiliana na changamoto za kimaadili kutokana na teknolojia kwa kupitia usimamizi wa kulingana na hali halisi, na namna gani AI kwa watu wote inatimizwa wakati pengo la kidijitali linapoendelea kupanuka.
"Maswali haya yanahitaji kuzingatiwa kwa umakini na kutoa majibu halisi kwa jumuiya nzima ya kimataifa," alisema. Xi amesisitiza hitaji la kufuata kanuni za ufunguaji mlango na kutafuta maendeleo kwa pamoja, kusukuma mbele maendeleo yanayotegemea uvumbuzi, kuongeza uelewa wa hatari na kuhakikisha usalama na udhibiti wa AI, kuhamasisha ujumuishaji na kuhimiza hali ya kufundishana kati ya ustaarabu mbalimbali, na kutetea mshikamano na kuboresha usimamizi wa Dunia.
"Lazima tufanye ushirikiano mpana wa kimataifa na kuzisaidia nchi za Dunia ya Kusini kuongeza uwezo, kuziba pengo la AI na la kidijitali, kuhimiza maendeleo endelevu, na kuzuia hali mpya isiyo na usawa ya kihistoria isitokee katika sekta ya AI," alisema. "China ikiwa nchi kubwa inayowajibika, siku zote inajitolea kutoa bidhaa za umma za kimataifa zinazohusiana na AI," alisema Xi, ambaye alitoa Pendekezo la Usimamizi wa AI Duniani mwaka 2023.

Roboti zikionekana kwenye Kituo cha Maonyesho na Mikutano cha Maonyesho ya Dunia cha Shanghai China. (Xinhua/Ding Ting)
Amesema kuanzishwa kwa Jumuiya ya Ushirikiano wa AI ya Dunia, ni uitikio mkubwa wa China kwa wito wa nchi za Dunia ya Kusini, na pia ni hatua muhimu ya jumuiya ya kimataifa ya kufanya juhudi za kuhimiza kwa maendeleo na usimamizi wa AI.

Wafanyakazi wakipanga mabanda ya maonyesho kwenye Kituo cha Maonyesho na Mikutano cha Maonyesho ya Dunia cha Shanghai China. (Xinhua/Ding Ting)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



