Waziri Mkuu wa China afanya mazungumzo na waziri mkuu wa Thailand

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 21, 2026

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Nchi ya Kifalme ya Thailand Anutin Charnvirakul, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Julai 20, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Nchi ya Kifalme ya Thailand Anutin Charnvirakul, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Julai 20, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)

BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Nchi ya Kifalme ya Thailand Anutin Charnvirakul ambaye yuko katika ziara yake ya kwanza rasmi nchini China mjini Beijing jana Jumatatu.

Waziri mkuu Li alisema kuwa China na Thailand ni majirani wa karibu wenye historia ndefu ya mawasiliano ya kirafiki, chini ya uelekezaji wa kimkakati wa viongozi wa nchi hizo mbili, ujenzi wa jumuiya ya China na Thailand yenye mustakabali wa pamoja unaendelea kwa kina na kuimarika kila mara, hali ambayo imefungua matarajio mapana zaidi kwa ushirikiano wa pande mbili.

Li amesema China inapenda kuenzi zaidi urafiki wa jadi na Thailand, kuongeza hali ya kuaminiana kisiasa, kuungana mkono zaidi, kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana katika sekta mbalimbali ufanyike kwenye ngazi ya juu zaidi, na kuongeza ustawi siku hadi siku kwa watu wa pande hizo mbili.

"China iko tayari wakati wote kuifanya mikakati ya maendeleo ihusiane na ile ya Thailand na kuungana mkono, kufuata ushirikiano wa sifa bora wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kudumisha mwelekeo mzuri wa ongezeko la biashara kati ya pande mbili, kupanua ushirikiano katika nyanja zinazoibuka, na kufanya juhudi za pamoja za kuhimiza ustawi kwa pamoja," Li ameongeza.

Ameelezea matumaini yake kwamba Thailand itatoa mazingira mazuri ya kibiashara kwa kampuni za China, na kuongeza kwamba pande hizo mbili zinapaswa kuimarisha zaidi ushirikiano katika utekelezaji wa sheria na usalama.

Kwa upande wake Anutin, amesema kwamba mkutano wa viongozi wakuu wa nchi hizo mbili mwaka jana umeingiza msukumo mpya katika uhusiano wa pande mbili, na Thailand inapenda kudumisha mawasiliano ya karibu kwenye ngazi ya juu na China, kutumia vya kutosha mfumo wa mazungumzo, kuhimiza ushirikiano katika sekta mbalimbali, na kujitahidi kujipatia mafanikio halisi zaidi katika uhusiano wa washirika wa pande mbili.

Amesema Thailand inafuata kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja, na kamwe haitaunga mkono kitendo chochote cha kuifanya "Taiwan ijitenge". Pia amedhihirisha kuwa Thailand itaongeza juhudi zake za kupambana na uhalifu wa kuvuka mipaka, na kujenga mazingira salama na mazuri kwa watalii wa China na kampuni za China.

Baada ya mazungumzo yao, viongozi hao wawili walishuhudia utiaji saini wa nyaraka kuhusu ushirikiano katika sekta za biashara, sayansi na teknolojia, elimu ya AI, safari kwenye anga ya juu na vyombo vya habari.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Nchi ya Kifalme ya Thailand Anutin Charnvirakul, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Julai 20, 2026. (Xinhua/Yin Bogu)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Nchi ya Kifalme ya Thailand Anutin Charnvirakul, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Julai 20, 2026. (Xinhua/Yin Bogu)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha