Lugha Nyingine
Wilaya ya Raohe mkoani Heilongjiang yaendeleza shughuli ya kijadi ya ufugaji nyuki kuwa kilimo cha kisasa cha kuweka mkazo wa chapa (6)
![]() |
| Mfugaji nyuki akitazama nyuki weusi kwenye eneo la ufugaji nyuki katika Wilaya ya Raohe, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, Julai 22, 2026. (Xinhua/Wang Song) |
Raohe ni wilaya moja ya mpakani katika Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, hali yake ya hewa na ya kijiografia inafaa sana kwa shughuli ya kufuga nyuki weusi. Hifadhi ya mazingira ya asili ya ngazi ya kitaifa ilianzishwa hapa mwaka 1997 ili kuhifadhi spishi ya nyuki weusi.
Kwa kutumia rasilimali zake za kipekee, wilaya hiyo ya Raohe imeendeleza shughuli ya ufugaji nyuki weusi kuwa nguzo ya kazi zake, na inafanya juhudi za kukuza shughuli ya kijadi ya ufugaji nyuki kuwa kilimo cha kisasa cha kuweka mkazo katika kukuza chapa.
Mpaka hivi sasa, hifadhi hiyo kwa jumla imekuwa na makundi ya nyuki 42,000, maeneo 431 ya kufugia nyuki, pamoja na watu 1,300 wanaoshughulikia ufugaji nyuki. Thamani ya jumla ya bidhaa za nyuki weusi za wilaya hiyo zikiwa ni pamoja na chapa za asali, jeli ya nyuki malkia na masega imezidi yuan bilioni 1.488 (dola za Marekani milioni 219.7).
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




