Mkutano wa ngazi ya mawaziri wa APEC wapitisha Taarifa ya Chengdu juu ya teknolojia za kidijitali na AI (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 24, 2026
Mkutano wa ngazi ya mawaziri wa APEC wapitisha Taarifa ya Chengdu juu ya teknolojia za kidijitali na AI
Washiriki wakihudhuria Mkutano wa ngazi ya Mawaziri wa APEC wa Mambo ya Kidijitali na AI 2026 mjini Chengdu, kusini magharibi mwa Mkoa wa Sichuan wa China, Julai 23, 2026. (Xinhua/Wang Xi)

CHENGDU - Mkutano wa ngazi ya Mawaziri wa APEC wa Mambo ya Kidijitali na AI 2026 umepitisha taarifa ya mawaziri huku pande zote zikikubaliana kuhimiza kwa pamoja teknolojia za kidijitali na AI ili kuiwezesha jumuiya ya Asia-Pasifiki, ambayo hutoa mfumo kazi kwa ajili ya kuzidisha ushirikiano katika nyanja hizo kwa miaka ijayo kwenye eneo hilo.

Mkutano huo wa ngazi ya mawaziri, ambao ni jukwaa muhimu kwa ajili ya kuhimiza ubadilishanaji uzoefu na ushirikiano katika sekta za teknolojia za kidijitali, za kupashana habari na mawasiliano katika eneo lote la Asia-Pasifiki, ulifanyika jana Alhamisi huko Chengdu, mji mkuu wa Mkoa wa Sichuan kusini magharibi mwa China, chini ya kaulimbiu ya "Teknolojia za Kidijitali na AI kwa Uwezeshaji wa Jumuiya ya Asia-Pasifiki."

Kuhusu matokeo ya mkutano huo, Waziri wa Viwanda na Teknolojia ya Kupashana Habari wa China Li Lecheng, ambaye aliongoza kikao cha mkutano huo, amebainisha kuwa mkutano huo umeweka msisitizo katika kuharakisha maendeleo ya miundombinu ya mawasiliano na mambo ya kompyuta.

Li amesema kwamba makubaliano yaliyofikiwa, hasa maelezo mahususi juu ya kuhimiza mabadiliko makubwa ya kidijitali na ya AI ya viwanda vya jadi na kuunga mkono biashara ndogo ndogo, za ukubwa mdogo na wa kati katika kutumia ipasavyo zana nyepesi za kidijitali ili kuongeza uwezo wao wa kushindana, yametoa njia za maendeleo zinazotilia maanani zaidi watu na za muktadha maalum kwa uchumi wa pande zote za Asia-Pasifiki.

"China itaendelea kutumia ipasavyo utaratibu wa APEC, kuimarisha ushirikiano na uchumi wa pande zote, kutekeleza maafikiano yaliyofikiwa kwenye mkutano huu, na kuzidisha ubadilishanaji uzoefu na ushirikiano," Li ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha