Wanahisabati Wachina Deng Yu na Wang Hong watumukiwa Nishani za Fields (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 24, 2026
Wanahisabati Wachina Deng Yu na Wang Hong watumukiwa Nishani za Fields
Mwanahisabati Mchina Wang Hong (wa tatu, kulia) akiwa ametunukiwa Nishani ya Fields kwenye hafla ya kufunguliwa kwa Mkutano wa Wanahisabati wa Kimamtaifa 2026, huko Philadelphia, Marekani, Julai 23, 2026. (Xinhua/Li Rui)

PHILADELPHIA, Marekani - Wanahisabati Wachina Deng Yu na Wang Hong wamepewa Nishani za Fields kwenye Mkutano wa Wanahisabati wa Kimataifa 2026 uliofunguliwa Philadelphia, Marekani jana Alhamisi, na hii ni mara ya kwanza kwa wanahisabati Wachina kupata heshima hiyo ya kifahari. Kwenye hafla ya kufunguliwa kwa mkutano uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Pennsylvania, Umoja wa Hisabati wa Kimataifa ulitangaza kwamba Deng ameshinda nishani kwa kazi yake katika partial differential equations (PDEs), na Wang ameshinda nishani kwa kazi yake katika uchambuzi wa harmoniki na nadharia ya kipimo cha kijiometri.

Deng amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya hafla hiyo, "Ni heshima kubwa kwa jina langu kuweza kuorodheshwa kwa kufuatia wanahisabati wote hao wakubwa ambao ninawasifu na kuwaheshimu sana siku zote. Huu ni utambuzi muhimu sana kwangu, kwa kazi yangu, kwa utafiti wa mimi na washirika wangu, na vilevile kwa nyanja ya PDE na elimu ya kipimo cha uwelekeo wa uwezekano ninayowakilisha."

"Utambuzi huo una umuhimu mkubwa sana kwa mimi na washirika wangu wengine," Wang amesema.

"Nimefurahi sana kwa Dkt. Deng na Dkt. Wang, na ninawapongeza wote wawili kwa furaha kubwa," mshindi wa Nishani ya Fields Efim Zelmanov ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.

"Sehemu muhimu ya elimu ya washindi hao wawili ilikamilishwa nchini China. Mafanikio yao makubwa ni utambuzi wenye nguvu kwa kazi ya kimsingi ya China inayoongezeka kwa kasi katika ulimwengu wa hisabati," Zelmanov ameongeza.

Deng alisoma kwanza katika Chuo Kikuu cha Beijing cha China kabla ya kuendelea na masomo katika Chuo Kikuu cha Teknolojia ya Massachusetts (MIT), na amepata Shahada ya Uzamivu (PhD) katika masomo ya Chuo Kikuu cha Princeton. Wang alipata shahada yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Beijing, shahada ya uzamili katika masomo ya Chuo Kikuu cha Paris-Saclay na Shahada ya Uzamivu (PhD) katika masomo ya Chuo kikuu cha MIT.

Deng ni profesa katika Chuo Kikuu cha Chicago. Wang ni profesa katika Taasisi ya Sayansi ya des Hautes Etudes nchini Ufaransa na Taasisi ya Courant katika Chuo Kikuu cha New York.

Kwa jumla kuna washindi wanne wa Nishani za Fields mwaka huu. Wengine wawili ni John Pardon, mtaalamu wa hisabati wa Marekani katika Chuo Kikuu cha Stony Brook; na Jacob Tsimerman, mtaalamu wa hisabati wa Canada katika Chuo Kikuu cha Toronto.

Nishani ya Fields ni tuzo ya juu ya hisabati ya kimataifa inayotolewa kila baada ya miaka minne kwa watafiti vijana wawili hadi wanne walio chini ya umri wa miaka 40 ili kusifu mafanikio yao bora ya hisabati katika kazi zilizopo na uwezo wao mkubwa kwa mafanikio ya baadaye.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha