Shughuli za uokoaji zaendelea kufuatia kutokea mafuriko mkoani Gansu Kaskazini Magharibi mwa China (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 27, 2026
Shughuli za uokoaji zaendelea kufuatia kutokea mafuriko mkoani Gansu Kaskazini Magharibi mwa China
Shughuli za uokoaji zikiendelea kwenye eneo lililoathiriwa na mafuriko kutoka milimani katika Wilaya ya Weiyuan mkoani Gansu, kaskazini magharibi mwa China, Julai 26, 2026. (Ofisi ya Usalama wa Umma ya Weiyuan/kupitia Xinhua)

Ofisi ya Makao Makuu ya Kitaifa ya Kuzuia Mafuriko na Kupambana na Ukame na Wizara ya Usimamizi wa Kukabiliana na Hali ya Dharura ya China (MEM) wametuma timu ya kazi kwenda Mkoa wa Gansu kaskazini magharibi mwa China jana Jumapili kuongoza juhudi za kutoa msaada za serikali ya mkoa huo baada ya mafuriko ya ghafla kusababisha vifo na majeruhi.

Wizara ya Usimamizi wa Kukabiliana na Hali ya Dharura imesema, makao makuu yameanzisha mwitikio wa dharura wa kuzuia mafuriko wa Daraja la 4 kwa mkoa huo.

Mafuriko kutoka milimani yaliyosababishwa na mvua kubwa ya ghafla yalitokea kwenye eneo la kivutio cha utalii katika Wilaya ya Weiyuan ya Mji wa Dingxi, jana Jumapili alasiri, na kusababisha watu 10 kufariki na wengine 23 kujeruhiwa hadi saa 12 jioni ya siku hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha