Mipango ya ushirikiano wa kimatibabu kati ya China na Afrika yazinduliwa nchini Ethiopia ili kuifanya huduma ya afya kuwa ya kisasa (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 28, 2026
Mipango ya ushirikiano wa kimatibabu kati ya China na Afrika yazinduliwa nchini Ethiopia ili kuifanya huduma ya afya kuwa ya kisasa
Rais wa Ethiopia Taye Atske Selassie akitoa hotuba kwenye hafla ya uzinduzi wa mipango ya ushirikiano wa kimatibabu katika Hospitali Kuu ya Silk Road, Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Julai 27, 2026. (Xinhua/Geng Xinning)

ADDIS ABABA - China na Afrika zimezindua mipango ya ushirikiano wa kimatibabu mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia jana Jumatatu, inayolenga kuzifanya huduma za afya ya umma barani humo kuwa za kisasa, ikiwa ni sehemu ya kuzidisha mifumo ya ushirikiano wa kivitendo wa afya ya umma kati ya China na Afrika.

Hafla hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na Hospitali ya Xiangya ya Chuo Kikuu cha Kusini Kati cha China, Hospitali Kuu ya Silk Road ya Addis Ababa, na Muungano wa Hospitali wa China na Afrika, imeshuhudia uzinduzi wa Mpango wa Ushirikiano kati ya China na Afrika kwa Tiba ya Upasuaji Kidogo, pamoja na uzinduzi wa Kituo cha Mafunzo ya Upasuaji kwa Roboti kati ya China na Afrika na Kituo cha Mafunzo ya Teknolojia ya Endoskopia kati ya China na Afrika.

Hafla hiyo, iliyofanyika katika Hospitali Kuu ya Silk Road katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, iliwakutanisha maofisa waandamizi wa serikali ya Ethiopia, wanadiplomasia wa China, vilevile wataalamu wa matibabu wa Afrika na China na wataalamu wa afya.

Akihutubia mkutano huo, Rais wa Ethiopia Taye Atske Selassie amesisitiza umuhimu mkubwa wa kuingiza teknolojia ya kisasa na wafanyakazi wenye ujuzi wa afya katika sekta ya afya ya umma.

Amesema kwamba kwa kutumia mbinu za hali ya juu za matibabu, mipango hiyo mipya iliyozinduliwa inawezesha utoaji wa huduma bora za afya ya umma kwa jamii za Ethiopia na zaidi, kote barani Afrika.

Rais huyo, haswa, amewapongeza wakufunzi na madaktari wa tiba wa China kwa kujitoa kwao katika kuhamisha ujuzi na maarifa, akieleza kuwa ni "muhimu katika kuboresha huduma zetu za afya, kujiteua wenyewe na teknolojia mpya, na kuwa waanzilishi kwa njia nyingi."

Balozi wa China nchini Ethiopia Chen Hai ameuelezea mpango huo wa ushirikiano kuwa ni hatua ya kivitendo na hatua halisi katika kutekeleza Hatua ya Ushirikiano wa Afya chini ya Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

"Katika wakati huu ambapo ushirikiano wa kivitendo kati ya China na Afrika unaendelea kuzidishwa na kutoa matokeo halisi katika sekta nyingi, ninafurahi sana kuona utaalamu na rasilimali za hali ya juu za matibabu za China zikifikia Afrika, na hasa Ethiopia," amesema.

Kwenye hafla hiyo, wanagenzi takribani 40 kutoka Sudan, Tanzania, Uganda, Ghana, Libya, na Ethiopia pia walishiriki katika programu ya kwanza ya mafunzo juu ya teknolojia ya endoskopia, ambayo yalitolewa na wataalamu wa China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha