Eneo la Mhimili wa Katikati wa Beijing lapata nguvu hai mpya katika maadhimisho ya miaka miwili tangu kuwa urithi wa Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 28, 2026
Eneo la Mhimili wa Katikati wa Beijing lapata nguvu hai mpya katika maadhimisho ya miaka miwili tangu kuwa urithi wa Dunia
Watu wakicheza mchezo wa kupiga teke jiànzi kwenye uwanja unaounganisha Minara ya Ngoma na Kengele, Beijing, mji mkuu wa China, Julai 27, 2026. (Xinhua/Zhang Xiaoyu)

Maadhimisho ya pili ya kuorodheshwa kwa Eneo la Mhimili wa Kati wa Beijing kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia wa UNESCO yalikuwa jana Julai 27.

Tangu kuorodheshwa kwake, mhimili huo wenye urefu wa kilomita 7.8 umeendelea kupata nguvu hai mpya, ukivutia watembeleaji wengi zaidi kujionea urithi wa kihistoria wa Beijing huku kukiwa na mchanganyiko wa usanifu wa kale na maisha ya kisasa, wakati huohuo ukileta Urithi huo wa Dunia karibu na maisha ya kila siku.

Mhimili huo wa Kati wa Beijing wenye kutoka kwenye Minara ya Kengele na Ngoma upande wa kaskazini hadi Lango la Yongdingmen upande wa kusini, unaonyesha mipango miji ya jadi ya China na hutumika kama eneo la uti wa mgongo la mji wa zamani. Ukibeba historia ya maendeleo ya mjini ya Beijing, ni ushuhudia wa mwendelezo wa ustaarabu wa China na unaonyesha mapitio ya hali mbalimbali ya mji mkuu huo wa China kapitia zama mbalimbali.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha