Lugha Nyingine
Timu ya tatu ya wataalamu wa matibabu wa China yawasili DRC kuunga mkono mapambano dhidi ya Ebola

Timu ya tatu ya wataalamu wa matibabu wa China ya kusaidia kazi ya kukabiliana na Ebola ikiwasili Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Agosti 1, 2026. (Xinhua)
KINSHASA –Jumamosi ya wiki iliyopita, timu ya tatu ya wataalamu wa matibabu wa China ya kusaidia kukabiliana na Ebola imewasili Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), timu hiyo itaunga mkono juhudi za nchi hiyo za kuimarisha kazi ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa.
Luku Maleyo Marius, mwakilishi wa wizara ya afya ya DRC, aliikaribisha timu hiyo katika uwanja wa ndege.Amesema hali mbaya ya Ebola bado inaendelea nchini DRC, na kazi za kuzuia na kudhibiti ugonjwa huo bado zinakabiliwa na shinikizo kubwa. Ameeleza kuwa kuwasili kwa wataalamu wa China kutatoa uungaji mkono wenye nguvu kwa ufuatiliaji wa hali ya maambukizi ya ugonjwa, kutibu wagonjwa na kufanya upimaji ndani ya maabara.
“DRC iko tayari wakati wote kuimarisha zaidi ushirikiano na China na kwa pamoja kuongeza uwezo wa kukabiliana na hali ya maambukizi ya ugonjwa,” ameongeza.
Yang Xiaochen, mkuu wa timu hiyo ya tatu ya wataalamu amesema, kwenye msingi wa kazi zilizofanywa na timu mbili za wataalamu wa China zilizoondoka, timu yake hiyo itaendelea kutoa msaada wa kiufundi kutokana na mahitaji ya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa, na kuongeza zaidi kubadilishana maoni na kufanya ushirikiano na idara za afya za DRC na washirika husika wa kimataifa.Yang amesema timu hiyo itachangia ujuzi wa taalamu wa China katika juhudi za kukomesha mapema iwezekanavyo maambukizi ya hivi sasa ya ugonjwa wa Ebola.

Timu ya tatu ya wataalamu wa matibabu wa China ya kusaidia mapambano dhidi ya Ebola wakiwasili Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Agosti 1, 2026. (Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



