Lugha Nyingine
Ethiopia yazindua kampeni ya nchi nzima ya kupanda miti milioni 800 kwa siku moja

Watu wakishiriki kwenye kampeni ya nchi nzima ya upandaji miti ikiwa ni sehemu ya Mpango mkuu wa Urithi wa Kijani wa nchi hiyo mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Agosti 3, 2026. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)
ADDIS ABABA - Mamilioni ya Waethiopia na raia wa kigeni nchini humo wameshiriki kwenye kampeni ya nchi nzima ya upandaji miti jana Jumatatu, wakilenga kupanda idadi ya kuvunja rekodi ya miche ya miti milioni 800 katika siku moja ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kitaifa ya upandaji miti.
Shughuli hiyo ya nchi nzima ni sehemu ya Mpango mkuu wa Urithi wa Kijani wa nchi hiyo, uliozinduliwa na Waziri Mkuu Abiy Ahmed mwaka 2019. Kama sehemu ya shughuli ya mwaka huu ya mpango huo, nchi hiyo ya Afrika Mashariki inalenga kupanda jumla ya miche ya miti zaidi ya bilioni 8 katika msimu wa mvua.
Wakati huu ambapo Ethiopia ikijitahidi kufikia azma yake ya kujenga uchumi wa kijani wenye kipato cha kati cha chini katika siku za usoni, mpango huo mkubwa wa upandaji miti unaoongozwa na serikali umeshika kasi katika miaka ya hivi karibuni.
Abiy amesema kwamba juhudi hizo za kila mwaka za nchi nzima za upandaji miti kwa siku moja ni "wakati ambapo Waethiopia kutoka nyanja zote za maisha wanakusanyika pamoja ili kuunda urithi wa kudumu kwa vizazi vijavyo."
"Miaka minane ya hatua thabiti. Mpango wa Urithi wa Kijani unaendelea kuimarika, ukichochewa na dhamira ya umma na imani ya pamoja kwamba, kwa pamoja, Waethiopia wanaweza kujenga mustakabali wa kijani na endelevu zaidi," Abiy ameandika kwenye ujumbe wake katika mtandao wa X, ambao hapo awali uliitwa Twitter, baada ya kupanda miche.
Kwa kuongezwa kwa miche mipya zaidi ya bilioni 8 mwaka huu, nchi hiyo inalenga kuvuka lengo kabambe la kupanda miti bilioni 50 tangu kuzinduliwa kwa Mpango wa Urithi wa Kijani mwaka 2019.

Watu wanashiriki kwenye kampeni ya nchi nzima ya upandaji miti kama sehemu ya Mpango mkuu wa Urithi wa Kijani wa nchi hiyo mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Agosti 3, 2026. (Xinhua/Geng Xinning)

Watu wanashiriki kwenye kampeni ya nchi nzima ya upandaji miti kama sehemu ya Mpango mkuu wa Urithi wa Kijani wa nchi hiyo mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Agosti 3, 2026. (Xinhua/Geng Xinning)

Jamaa akishiriki kwenye kampeni ya nchi nzima ya upandaji miti kama sehemu ya Mpango mkuu wa Urithi wa Kijani wa nchi hiyo mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Agosti 3, 2026. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



