Lugha Nyingine
Mradi wa kituo cha kitaifa cha upasuaji kinachojengwa kwa msaada wa China wawekewa jiwe la msingi nchini Msumbiji

Rais wa Msumbiji Daniel Chapo akishiriki kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa Mradi wa Kituo cha Kitaifa cha Upasuaji kinachojengwa kwa msaada wa China mjini Maputo, Msumbiji, Agosti 3, 2026. (Picha na Mendes Mondlane/Xinhua)
MAPUTO - Hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa Kituo cha Kitaifa cha Upasuaji unaofanywa kwa msaada wa China imefanyika huko Maputo, Msumbiji jana Jumatatu.
Kituo hicho kitajengwa ndani ya Hospitali Kuu ya Maputo, kikihusisha jengo moja la kituo cha upasuaji na majengo mawili ya huduma, na eneo la jumla la ujenzi huo unafikia mita za mraba zaidi ya 20,000.
Kituo hicho cha upasuaji cha ghorofa nane, chenye ghorofa moja chini ya ardhi, kitakuwa na huduma za dharura na kiwewe, vitengo vya picha za matibabu, dawa, maabara, vyumba 14 vya upasuaji, wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa kina yenye vitanda 19 vya wagonjwa wenye hali mbaya na vitanda 456 vya wagonjwa wa kulazwa.
Akihutubia hafla hiyo, Rais wa Msumbiji Daniel Chapo amesema uwekaji huo wa jiwe la msingi unamaanisha mwanzo wa hatua mpya katika uwezo wa Msumbiji wa kuokoa maisha na kutibu magonjwa magumu, na kuwezesha Wamsumbiji zaidi kupata huduma maalum ya matibabu ndani ya nchi yao.
Akizielezea Msumbiji na China kuwa ni nchi ndugu, Chapo amesema serikali ya Msumbiji inatarajia kufanya ushirikiano na serikali ya China ili kukomesha hali ya Wamsumbiji kusafiri nje ya nchi kutafuta huduma bora ya matibabu.
Amesema nchi mbili Msumbiji na China zimejenga uhusiano imara wa wenzi katika miongo kadhaa iliyopita, uhusiano huo unaendelea kwenye msingi wa kuheshimiana, kuaminiana kisiasa na juhudi za pamoja katika kutafuta mpango wa maendeleo kwa ajili ya manufaa ya watu wao.
"Urafiki huu kwa mara nyingine tena unabadilika kuwa uwekezaji ambao utakuwa na matokeo mazauri ya moja kwa moja kwa maisha ya maelfu ya familia za Wamsumbiji," Chapo amesema, akiongeza kuwa anaamini mradi huo utakuwa " alama nyingine muhimu" ya urafiki na ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili, hasa katika nyanja ya afya ya umma."
Balozi wa China nchini Msumbiji Zheng Xuan amesema China siku zote inaweka umuhimu wa kwanza juu ya afya ya watu na kutilia maanani zaidi kuunga mkono maendeleo ya sekta ya afya ya Msumbiji.
Amesema China siku zote inashirikiana na Msumbiji kwa kuboresha ustawi wa watu wao kwa kupitia kutuma timu za madaktari, kutoa mafunzo ya matibabu na kutoa zana na vifaa vya matibabu na dawa.

Rais wa Msumbiji Daniel Chapo akihutubia hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa Ujenzi wa Kituo cha Kitaifa cha Upasuaji unaofanywa kwa msaada wa China mjini Maputo, Msumbiji, Agosti 3, 2026. (Picha na Mendes Mondlane/Xinhua)

Rais wa Msumbiji Daniel Chapo akihudhuria hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa Ujenzi wa Kituo cha Kitaifa cha Upasuaji unaofanywa kwa msaada wa China mjini Maputo, Msumbiji, Agosti 3, 2026. (Picha na Mendes Mondlane/Xinhua)

Rais wa Msumbiji Daniel Chapo (wa pili kulia) akisikiliza maelezo ya Mradi wa Kituo cha Kitaifa cha Upasuaji kinachojengwa kwa msaada wa China kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa mradi huo mjini Maputo, Msumbiji, Agosti 3, 2026. (Xinhua/Liu Jie)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



