Duka la kwanza la kujaribu na kupata huduma za roboti 6S mjini Qingdao, China lafunguliwa (8)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 12, 2026
Duka la kwanza la kujaribu na kupata huduma za roboti 6S mjini Qingdao, China lafunguliwa
Watu wakitazama roboti ikifanya onesho ndani ya duka la kujaribu na kupata huduma za roboti 6S mjini Qingdao, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Agosti 11, 2026. (Xinhua/Li Ziheng)

Hivi karibuni, Duka la kwanza la kujaribu na kupata huduma za roboti 6S katika Mji wa Qingdao, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China lilifunguliwa, na kuvutia idadi kubwa ya wanunuzi kutembelea ili kujaribu na kuelewa namna ya kutumia roboti. Duka hilo linajumuisha kazi kuu sita za mauzo, vipuri, huduma, utafiti, kukodisha na kukidhi mahitaji ya mtu mahsusi, ili kusaidia zaidi matumizi ya roboti yawe hali ya kawaida katika maisha ya watu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha