Ndege C919 iliyoundwa na China yenyewe yakamilisha safari ya kwanza ya kimataifa ya kibiashara, yatua Ulan Bator, Mongolia (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 13, 2026
Ndege C919 iliyoundwa na China yenyewe yakamilisha safari ya kwanza ya kimataifa ya kibiashara, yatua Ulan Bator, Mongolia

ULAN BATOR - Ndege kubwa ya abiria C919 iliyoundwa na China yenyewe imetua salama katika uwanja mpya wa ndege wa Ulan Bator nchini Mongolia Jumatano alasiri baada ya kuondoka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital, ikiashiria kukamilika kwa safari ya kwanza kupangwa ya kimataifa ya kibiashara ya abiria kwa ndege hiyo.

Hafla kubwa ya saluti ya lango la maji ilifanyika katika uwanja huo wa ndege. Abiria walishuka mmoja baada ya mwingine kutoka kwenye ndege hiyo, wakatazama onyesho la kipekee la ngoma ya jadi, na walipokelewa na msafara wa wahudumu waliokuwa wamevalia mavazi ya kijadi ya Kabila la Wamongolia.

Njia hiyo ya China-Mongolia ni njia ya kwanza ya kimataifa kufunguliwa baada ya C919 kuanza kutoa huduma za kibiashara, ikiashiria kuingia rasmi kwa ndege hiyo C919 iliyoundwa na China yenyewe katika awamu mpya ya utoaji huduma wenye ratiba ya kawaida kimataifa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, njia hiyo ya kimataifa inaendeshwa chini ya safari za ndege No. CA723/CA724, huku safari za ndege zikipangwa kila siku katika huduma yenye ratiba ya kawaida.

C919 ambayo ni ndege kubwa ya kwanza ya abiria ya jeti iliyoundwa na China yenyewe kwa matumizi ya kiraia, imekuwa ikiendeshwa kwa mafanikio katika njia mbalimbali za ndani ya China tangu ianze kutoa huduma kibiashara. Imepata utambuzi mkubwa sokoni kutokana na ufanisi wake wa kuaminika kwenye safari, mazingira na hali bora ndani yake, na viwango tulivu vya kiusalama.

Uendeshaji wa safari hiyo ya ndege katika njia hiyo ya kimataifa ya China-Mongolia unaonyesha kwamba C919 imefaulu uthibitishaji wa viwango vya uendeshaji kwa usafiri wa anga wa kiraia wa kimataifa kati ya pande mbili, na hivyo kuruhusiwa kufanya uendeshaji wa kawaida wa safari za kimataifa za kibiashara za abiria.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha