Lugha Nyingine
Maelfu ya watu wahamishwa kutokana na mafuriko ya maji ya mto yaliyosabibishwa na mvua kubwa katikati mwa China (4)
![]() |
| Picha ikionyesha kazi ya ukarabati ikiendelea kwenye sehemu iliyobomoka ya boma la Mto Beiru katika Wilaya ya Jiaxian, Mkoa wa Henan, katikati mwa China, Agosti 13, 2026. (Xinhua/Yang Jinxin) |
ZHENGZHOU - Serikali za mitaa ya Mkoa wa Henan katikati mwa China zimesema, maelfu ya watu wamehamishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kwa siku kadhaa kusababisha mafuriko ya maji ya mito na kubomoka kwa sehemu ya boma la mto.
Katika Mji wa Pingdingshan, watu zaidi ya 2,000 wamehamishiwa mahali salama baada ya kubomoka kwa sehemu ya boma la Mto Beiru wa Wilaya ya Jiaxian Jumatano usiku kutokana na athari mbaya ya mvua kubwa kupita kiasi na mafuriko makubwa ya maji yaliyoondolewa kutoka kwenye mabwawa ya juu ya mto. Serikali za mitaa zimesema, hakuna vifo au majeruhi walioripotiwa hadi sasa.
Ripoti husika imesema, sehemu iliyobomoka ya boma ina upana wa mita zaidi ya 40. Na viwango vya maji vilikuwa vinapungua kufikia jana Alhamisi asubuhi, wakati huohuo kazi ya ukarabati ilikuwa inaendelea ili kuziba pengo hilo.
Katika Mji wa Luohe, watu zaidi ya 4,500 kutoka vijiji 10 wamehamishwa kutokana na hali wasiwasi inayozidi kuongezeka juu ya uwezekano wa kutokea mafuriko ya mto.
Kutoka Jumatatu alasiri hadi Jumatano alasiri wiki hii, mji huo ulirekodi wastani wa mvua iliyonyesha wa milimita 270.1, na kiwango kikubwa zaidi cha mvua kilifikia milimita 434.2, hali ambayo iliifanya ofisi husika kutoa mwitikio wa ngazi ya juu zaidi wa kukabiliana na hali ya dharura ya kudhibiti mafuriko.
Kituo cha Kitaifa cha Hali ya Hewa cha China kilitoa tena tahadhari ya njano kwa mvua kubwa jana Alhamisi, kikitabiri kunyesha mvua kubwa katika maeneo kadhaa ya mikoa ya Henan na Hubei.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




