Lugha Nyingine
Tembo mwitu wa Asia wapewa huduma bora zaidi katika Mkoa wa Yunnan kusini-magharibi mwa China
KUNMING - "Familia yenye pua fupi" ya tembo mwitu wa Asia ilivutia ufuatiliaji mkubwa wa kimataifa mwaka 2021 baada ya kuzunguka kilomita zaidi ya 1,400 katika Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China. Ilirudi kwenye makazi yake ya kawaida ikiwa na wanafamilia 14. Kutokana na kukumbatia ndama wawili waliozaliwa mwaka huu, idadi ya wanafamilia wa tembo hao imeongezeka hadi 21.
Mkoa huo wa Yunnan umeendeleza mbinu kapambe ya uhifadhi wa tembo hao wa Asia ambao unachanganya urejeshaji makazi, makazi yaliyounganishwa, ufuatiliaji wa kisayansi na tahadhari ya mapema, ushiriki wa jamii na ushirikiano wa kuvuka mipaka. Mkoa huo pia ni nyumbani kwa Kituo cha Uzalianaji na Uokoaji wa Tembo wa Asia cha Xishuangbanna, ambacho kimeokoa na kurejesha utimamu wa afya wa tembo mwitu wa Asia zaidi ya 30 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009.
China imeanzisha hifadhi 11 za mazingira ya asili zinazoenea eneo lenye ukubwa wa jumla wa kilomita za mraba 5,098 kwenye makazi mbalimbali ya tembo mwitu hao wa Asia. Idadi ya tembo mwitu wa Asia ya nchi hiyo imeongezeka kutoka takriban 150 katika miaka ya 1980 hadi karibu 400 leo hii.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




