China yarusha Roketi ya Changzheng No.12 iliyobeba kundi jipya la satalaiti za intaneti

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 17, 2026
China yarusha Roketi ya Changzheng No.12 iliyobeba kundi jipya la satalaiti za intaneti
Roketi ya Changzheng No.12 iliyobeba kundi la 24 la satalaiti za intaneti za obiti ya chini ikirushwa kutoka eneo la kurushia vyombo vya kibiashara katika Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Agosti 16, 2026. (Picha na Liu Jianqiu/Xinhua)

WENCHANG, Hainan - China imerusha kundi jipya la satalaiti za intaneti kwenda ndani ya obiti jana Jumapili kutoka eneo la kurushia vyombo vya kibiashara kwenye anga ya juu katika mkoa wa kisiwa wa Hainan, kusini mwa China.

Satalaiti hizo, ambazo ni za kundi la 24 la satalaiti za intaneti za obiti ya chini, zikibebwa na roketi ya Changzheng No. 12 zimerushwa majira ya saa 6:10 mchana (Saa za Beijing) na kuingia kwa mafanikio kwenye obiti zao kwa mpango uliowekwa.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha