Xi Jinping atoa wito wa kusukuma mbele ujamaa wenye umaalum wa China katika wakati wa kumbukumbu ya miaka mia moja ya kiongozi marehemu Jiang Zemin

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 18, 2026

Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu kwenye mkutano mkuu wa kumbukumbu ya miaka mia moja ya kuzaliwa kwa kiongozi marehemu Jiang Zemin kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Agosti 17, 2026. (Xinhua/Li Xiang)

Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu kwenye mkutano mkuu wa kumbukumbu ya miaka mia moja ya kuzaliwa kwa kiongozi marehemu Jiang Zemin kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Agosti 17, 2026. (Xinhua/Li Xiang)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amesifu sana "mchango usioweza kufutika" alioutoa kiongozi marehemu Jiang Zemin, na ametoa wito wa kutaka Chama kizima na watu wa makabila yote ya China kusukuma mbele mambo ya ujamaa wenye umaalum wa China.

Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ameyasema hayo katika hotuba yake ya jana Jumatatu kwenye mkutano mkuu wa kumbukumbu ya miaka mia moja ya kuzaliwa kwa Jiang uliofanyika katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.

"Tunatoa heshima za juu sana kwa mafanikio yake makubwa, na kujifunza kutoka kwa mwenendo wake uliosifiwa," Xi amesema, na kutoa wito wa kuendelea kufanya juhudi za kujenga maisha mazuri zaidi kwa ajili ya watu wa China na kuandika ukurasa wa kung'ara zaidi kwa taifa la China.

Katika hotuba yake ya kutoa heshima, Xi amemwelezea Jiang kuwa ni mpiganaji mkomunisti aliyejaribiwa katika kukabiliana na changamoto kwa muda mrefu, na ni kiongozi bora wa mambo ya ujamaa wenye umaalum wa China. Amesema Jiang alikuwa kiongozi mkuu wa kizazi cha tatu cha uongozi wa pamoja wa kamati kuu ya Chama na mwanzilishi mkuu wa fikra muhimu ya Uwakilishi Mtatu. "Jiang alitoa mchango muhimu usioweza kufutika katika kulinda mambo ya ujamaa wenye umaalum wa China, na alipata mafanikio mapya kwenye mageuzi na ufunguaji mlango katika mambo yote, kufikia wastani wa ustawi wa jumla wa maisha ya watu na kusukuma mbele kwa mafanikio mambo ya ujamaa wenye umaalum wa China kuingia karne ya 21," Xi amesema.

Xi amesifu sana imani thabiti ya Jiang kwa matumaini ya ukomunisti na kujitolea kwake kwa Chama na wananchi, na ametoa wito kwa wanachama wa Chama kupata nguvu ya hamasa kutoka kwenye imani yake thabiti ya kisiasa.

Jiang alizaliwa Agosti 1926 huko Yangzhou mkoani Jiangsu. Mwaka 1989, alichaguliwa kuwa katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC. Alifariki mwaka 2022 akiwa na umri wa miaka 96.

Takriban watu 6,000 walihudhuria mkutano huo wa kumbukumbu wa Jumatatu. Mkutano huo uliongozwa na Li Qiang, na Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, na Li Xi -- wote wakiwa wajumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC-- walihudhuria kwenye mkutano huo pamoja na Makamu Rais Han Zheng.

Xi na viongozi wengine walikutana na wanafamilia wa Jiang na kupiga picha pamoja nao kabla ya mkutano huo kuanza.

Viongozi wa chama na serikali Xi Jinping, Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi, na Han Zheng wakihudhuria mkutano mkuu wa kumbukumbu ya miaka mia moja ya kuzaliwa kwa kiongozi marehemu Jiang Zemin kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Agosti 17, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)

Viongozi wa chama na serikali Xi Jinping, Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi, na Han Zheng wakihudhuria mkutano mkuu wa kumbukumbu ya miaka mia moja ya kuzaliwa kwa kiongozi marehemu Jiang Zemin kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Agosti 17, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)

Mkutano mkuu wa kumbukumbu ya miaka mia moja ya kuzaliwa kwa kiongozi marehemu Jiang Zemin ukifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Agosti 17, 2026. (Xinhua/Yue Yuewei)

Mkutano mkuu wa kumbukumbu ya miaka mia moja ya kuzaliwa kwa kiongozi marehemu Jiang Zemin ukifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Agosti 17, 2026. (Xinhua/Yue Yuewei)

Mkutano mkuu wa kumbukumbu ya miaka mia moja ya kuzaliwa kwa kiongozi marehemu Jiang Zemin ukifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Agosti 17, 2026. (Xinhua/Li Xiang)

Mkutano mkuu wa kumbukumbu ya miaka mia moja ya kuzaliwa kwa kiongozi marehemu Jiang Zemin ukifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Agosti 17, 2026. (Xinhua/Li Xiang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha