Lugha Nyingine
Mhifadhi Mchina afuatilia namna ya ulinzi wa wanyamapori unaotegemea jamii nchini Kenya

Zhuo Qiang (kushoto) akizungumza na Simon Msago, kiongozi wa jamii ya Wamasai, Ngoswani, Narok, Kenya, Agosti 12, 2026. (Xinhua/Liu Qiong)
NAIROBI - Alfajiri kunapopambazuka kwenye Hifadhi ya Ol Kinyei katika mfumo-ikolojia wa Maasai Mara nchini Kenya, walinzi wa hifadhi hiyo tayari wanapita katikati ya mbuga ili kubaini dalili za uingiaji bila idhini na ujangili wakati huohuo wakifuatilia kwa karibu wanyamapori.
Miongoni mwao ni mhifadhi Mchina Zhuo Qiang, mwenye jina la utani la "Simba". Kwake, utaratibu huo wa asubuhi na mapema unachochewa na dhamira pana ya kufanikisha kuishi kwa pamoja kwa binadamu na wanyamapori.
Mwaka 2010, Zhuo aliacha kazi yake nchini China akiwa na umri wa miaka 37 na kuanza njia ambayo haikuwa na watu wanaoifuata: kutafuta namna ya uhifadhi wa wanyamapori nchini Kenya.
Bila mafunzo ya kitaalamu katika uhifadhi wa wanyamapori, alijikuta katika eneo hilo, ambalo wakati huo lilikuwa linatawaliwa na mashirika ya Magharibi na watendaji wenyeji.
Lakini Zhuo aliamua kubaki. "Nilitaka kuthibitisha kwamba watu wa China wanaweza pia kufanya uhifadhi wa wanyamapori," amesema.
Awali, Zhuo aliona uhifadhi kwa kiasi kikubwa kupitia lenzi ya sayansi ya wanyamapori: kufanya kazi mbugani, kufanya stadi za wanyama na kukusanya takwimu.
Kuishi na kufanya kazi na jamii za Wamasai kulibadilisha mtazamo huo. "Hatima ya wanyamapori ilikuwa imefungamana kwa karibu na watu wanaochangia nao ardhi moja," amesema.
Katika mfumo-ikolojia wa Maasai Mara, ufugaji wa mifugo umeunganishwa kwa kina sana na maisha ya kila siku ya jamii za wafugaji. "Kama watu wenyeji wataombwa kuachana na ufugaji wa mifugo yao lakini hawapewi chanzo mbadala cha mapato, uhifadhi hauwezi kuwa endelevu," Zhuo amesema.
Kanuni hiyo iliweka msingi wa kazi yake na jamii ya wenyeji katika kuanzisha Hifadhi ya Ol Kinyei.
Zhuo amesema eneo hilo lilikuwa limeathiriwa na ufugaji kupita kiasi kwa muda mrefu, huku mimea na ardhi yenyewe vikizorota. Amesema, chini ya mfumo wa uhifadhi, ardhi ya malisho huko ilikodishwa na kurejeshwa hatua kwa hatua katika hali yake ya awali, hali ambayo iliruhusu mimea kuota tena na kujenga makazi yanayofaa zaidi kwa wanyamapori.
Wakati huo huo, kaya zinazoshiriki katika mpango huo hupokea mapato ya kukodisha ardhi na zinapata kazi kama vile kuwa walinzi wa hifadhi na wafanyakazi wa utalii. Mapato yao ya wastani kwa mwaka yameongezeka kutoka dola takriban 500 za Marekani hadi dola takriban 3,700, kwa mujibu wa Zhuo.
Baadhi ya wakazi kutoka jamii zinazozunguka pia walijifunza kutokana na uzoefu huo na kupeleka mbinu hiyo katika maeneo yao ya malisho.
Zhao amesema siku hizi, hifadhi 26 za kibinafsi zimeanzishwa kuzunguka Hifadhi ya Taifa ya Maasai Mara, zikienea kwenye eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba takriban 1,600.
Anaamini mtandao wa hifadhi za jamii hutoa nafasi ya ziada salama kwa wanyamapori kujongea na kuishi, na kupanua juhudi za uhifadhi kwenda zaidi ya mipaka ya hifadhi moja ya taifa na kuingia katika jamii zinazozunguka.
Simon Msago, kiongozi wa jamii ya Maasai huko Ngoswani, amesema kazi ya Zhuo imehamasisha wakazi wengi kuchukua jukumu kubwa katika uhifadhi.

Zhuo Qiang (C) akitazama kuku wanaofugwa na wakazi wenyeji, Narok, Kenya, Agosti 12, 2026. (Xinhua/Liu Qiong)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



