Lugha Nyingine
Kufungua Pazia | Sehemu ya 7: Ni kitu gani peasi moja linafichua kuhusu mustakabali wa kilimo
Maelezo ya Mhariri:
Kipindi cha “Kufungua Pazia” kinatumia simulizi halisi na mazingira ya kila siku kuelezea mantiki ya maendeleo nyuma ya Mpango wa 15 wa Miaka Mitano wa China. Kupitia simulizi za viwandani, watu na mambo halisi yaliyotokea, kinawapa watazamaji duniani mtazamo unaohusiana na kufikika zaidi kuhusu hatua inayofuata ya maendeleo ya China.
Katika sehemu ya 7 ya “Kufungua Pazia,” Mina anatembelea Wilaya ya Dangshan mkoani Anhui, Mashariki mwa China, ili kuchunguza mabadiliko makubwa ya kilimo cha kisasa, akichukua tasnia ya peasi wilayani humo kama mfano wakilishi.
Akiwa Dangshan, anakutana na Lin Yuan, mjasiliamali kijana ambaye amerudi nyumbani ambako ni chimbuko lake ili kubadilisha kilimo cha jadi kuwa cha kisasa kwa kutumia teknolojia janja. Hata hivyo, juhudi zake zilikutana na mashaka na upingaji kutoka kwa wakulima wenyeji, hali ambayo ilionesha umuhimu wa kujenga imani wakati wa mageuzi ya kilimo.
Kadri uchunguzi wake ulivyokuwa ukiendelea, Mina anakuja kutambua kuwa peasi moja la Dangshan linawakilisha mbali zaidi ya bidhaa moja ya kilimo. Nyuma yake kuna mfumo jumuishi unaojumuisha uvumbuzi wa mbegu, vifaa janja vya kilimo, usimamizi wa kidijitali na usambazaji wa kisasa sokoni.
Msingi wa maendeleo ya kilimo cha kisasa si teknolojia yenyewe, au “nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora” peke yake, bali ni kama nguvu hizo mpya za uzalishaji na mbinu husika za uzalishaji vinaweza au la kubadilisha kiukweli mifumo ya kilimo, kupata imani ya wakulima na kubadilishwa kuwa uwezo wa ushindani.
Mwongozo wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030) wa China unasema kuwa China itakipa kipaumbile kilimo na maendeleo vijijini, kuimarisha mifumo ya muda mrefu kwa ustawishaji wa vijiji wa pande zote na kuharakisha maendeleo ya kilimo cha kisasa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



