Lugha Nyingine
Xi atoa wito wa kuongeza ushirikiano kati ya China na Ecuador katika mikakati ya maendeleo

Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Ecuador Daniel Roy-Gilchrist Noboa Azín, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Agosti 18, 2026. (Xinhua/Li Xiang)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping jana Jumanne wakati akifanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Ecuador Daniel Roy-Gilchrist Noboa Azín ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China kuanzia Agosti 16 hadi 23, amesisitiza kwamba China na Ecuador zinapaswa kuimarisha ushirikiano katika mikakati yao ya maendeleo na kutekeleza mpango wa ushirikiano wa kujenga kwa pamoja Ukanda Mmoja, Njia Moja.
"Nchi zetu mbili zinapaswa kuhimiza miradi ya ushirikiano katika sekta za nishati, madini, miundombinu, na mambo ya fedha, na kufanya juhudi za kutafuta namna ya kushirikiana katika maeneo ya uchumi wa kidijitali, maendeleo ya kijani, nishati mpya na AI," Xi amesema.
Xi amesema China inaheshimu na kuunga mkono Ecuador katika kutafuta njia ya maendeleo inayolingana na hali ya nchi yake yenyewe. Amesema China inapenda kuongeza mawasiliano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na serikali, mabunge ya utungaji sheria, na vyama vya kisiasa, na kunufaika pamoja zaidi na uzoefu juu ya utawala.
Rais huyo wa China amezihimiza pande zote mbili kuendelea kufungua uwezekano wa makubaliano ya biashara huria ili faida zake ziweze kunufaisha zaidi viwanda na watumiaji.
Pia ameeleza nia ya China ya kushirikiana na Ecuador katika maeneo ya huduma za afya, kupunguza umaskini, kuzuia na kupunguza athari za maafa ya kimaumbile, na kuunga mkono maendeleo ya nchi ya Ecuador.
Rais Noboa amesema China ni mshirika muhimu na rafiki wa Ecuador, na uhusiano wa pande mbili umeingia katika kipindi kipya na kuleta manufaa halisi kwa watu wa pande hizo mbili.
Amesema Ecuador inapenda kuzidisha hali ya kuaminiana kisiasa na China, kuiunga mkono China kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi, na inaheshimu msimamo wa China juu ya suala la Taiwan.
Amesema Ecuador itapanua mauzo yake ya nje kwa China, na inakaribisha kampuni zaidi za China kuwekeza na kufanya shughuli zao nchini Ecuador, kwani hii inatarajiwa kusaidia kuongeza ustawi wa watu na kuhimiza maendeleo ya nchi hiyo.
Marais hao wawili walibadilishana maoni juu ya hali katika eneo la Latini Amerika na Karibeani.
Kabla ya mazungumzo yao kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Xi alifanya hafla ya kumkaribisha Noboa. Xi pia aliandaa dhifa ya kumkaribisha wakati wa jioni.

Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Ecuador Daniel Roy-Gilchrist Noboa Azín, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Agosti 18, 2026. (Xinhua/Li Xiang)

Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Ecuador Daniel Roy-Gilchrist Noboa Azín, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Agosti 18, 2026. (Xinhua/Zhang Ling)

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Ecuador Daniel Roy-Gilchrist Noboa Azín kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, Agosti 18, 2026. (Xinhua/Liu Bin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



