Iran yakataa taarifa ya UAE juu ya makombora "yaliyorushwa kutoka Iran"; UAE yasimamisha biashara na Iran

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 19, 2026

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baghaei akizungumza kwenye mkutano wa wiki na waandishi wa habari, Tehran, Iran, Agosti 17, 2026. (Xinhua/Shadati)

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baghaei akizungumza kwenye mkutano wa wiki na waandishi wa habari, Tehran, Iran, Agosti 17, 2026. (Xinhua/Shadati)

TEHRAN - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baghaei amekataa taarifa ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwamba makombora mawili ya balestiki yalirushwa jana Jumanne kutoka Iran kuelekea UAE.

Baghaei ametoa taarifa hiyo ya kukanusha mapema leo Jumatano, akisema tabia ya UAE inakinzana na kanuni ya ujirani mwema na imevuruga juhudi zinazoendelea za kuhimiza kuaminiana miongoni mwa nchi za kikanda na kuzuia kuongezeka kwa hali ya ukosefu wa usalama.

Picha hii iliyopigwa Septemba 3, 2024 ikionyesha mwonekano wa ikulu ya rais, Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu. (Xinhua/Sui Xiankai)

Picha hii iliyopigwa Septemba 3, 2024 ikionyesha mwonekano wa ikulu ya rais, Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu. (Xinhua/Sui Xiankai)

Ametoa wito kwa nchi za kikanda kujiepusha kutoa shutuma "zisizo na msingi" "kutokana na mambo magumu yaliyopo yanayosababishwa na vitendo viovu vinavyoendelea kufanywa na Marekani na Israel dhidi ya amani na usalama katika eneo hilo."

Wizara ya Ulinzi ya UAE ilisema jana Jumanne kwamba mifumo yake ya ulinzi wa anga ilibaini makombora mawili ya balestiki yaliyorushwa kutoka Iran kuelekea nchini humo, ikiongeza kwamba makombora hayo yalikuwa yanalenga vyombo vya usafiri wa baharini.

Wizara hiyo ilisema kwamba kombora la kwanza lilianguka nje ya maji ya eneo la UAE, wakati la pili lilianguka ndani ya maji ya eneo la nchi hiyo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya UAE imesema mapema leo Jumatano kwamba UAE imesimamisha biashara, mabadilishano ya kibiashara na miamala yote ya kifedha na Iran hadi itakapotangazwa tena, ikirejelea "kupamba moto kwa mashambulizi ya kikanda kunakodhoofisha amani na usalama wa kikanda na kimataifa."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha