Mjumbe wa UN atoa wito wa utashi wa kisiasa ili kusukuma mbele mchakato wa kisiasa wa Libya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 19, 2026

UMOJA WA MATAIFA - Mjumbe mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) wa masuala ya Libya ametoa wito wa utashi wa kisiasa ili kusukuma mbele mchakato wa kisiasa nchini Libya.

“Mpango wa kisiasa unaowezeshwa na Umoja wa Mataifa umepiga hatua muhimu. Hata hivyo, hatua hiyo haihitaji pekee juhudi za Ujumbe wa Uungaji Mkono wa UN nchini Libya (UNSMIL), bali pia utashi endelevu wa wadau wa kisiasa wa Libya kushiriki kiujenzi,” amesema Hanna Tetteh, mjumbe maalum wa katibu mkuu wa UN wa masuala ya Libya na mkuu wa UNSMIL.

Tetteh alitangaza mpango huo wa kisiasa mwaka mmoja uliopita, ambao umejengwa kuzunguka nguzo tatu kuu: mfumokazi wa uchaguzi wa rais na wabunge, kuendeleza uunganishaji wa taasisi kupitia serikali mpya iliyoungana, na mazungumzo yaliyopangiliwa kwa utaratibu.

“Haja ya kusukuma mbele mchakato wa kisiasa wa Libya inabaki kuwa muhimu. Kukatika kwa umeme kwa hivi karibuni na kutoridhika kwa umma, kulikozidishwa na wimbi la joto la muda mrefu, kumedhihirisha madhara ya mgawanyiko wa taasisi, uchepushaji mkubwa wa rasilimali za umma, uwekezaji wa chini na ufanyaji maamuzi usioratibiwa, ambavyo vyote kimsingi ni kushindwa kwa utawala,” amesema.

Tetteh amesema hiyo ndiyo maana mchakato wa kisiasa unahusu zaidi ya kuziba pengo kati ya pande zenye tofauti za kisiasa bali ni kuhusu kurejesha uwezo wa serikali katika kuhudumia watu wake, kusimamia rasilimali zake kwa uwajibikaji chini ya taasisi zinazounganishwa, kutoa usalama na kujenga uhimilivu ili kukabiliana na hatari mbalimbali ambazo inaweza kukumbana nazo.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha