Lugha Nyingine
China yampongeza Hakainde Hichilema kwa kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa rais nchini Zambia
(CRI Online) Agosti 19, 2026
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Lin Jian amesema kwamba, China inampongeza Rais wa Zambia Hakainde Hichilema kwa kuchaguliwa tena kushika wadhifa huo.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Jumanne Lin amesema kwamba China inaweka umuhimu mkubwa katika kuendeleza uhusiano na Zambia, na iko tayari kushirikiana na serikali mpya ya Zambia kuimarisha kwa kina uhusiano wa washirika wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili, na kuleta manufaa makubwa zaidi kwa watu wao.
Tume ya Uchaguzi ya Zambia jana Jumanne ilimtangaza rais huyo aliye madarakani Hichilema kuwa ni mshindi katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2026.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



