Lugha Nyingine
Kufungua Pazia | Sehemu ya 8: Kama milima na mito ikipoteza rangi zao, kwa namna gani tunaweza kuangazia mustakabali?
Maelezo ya Mhariri:
Kipindi cha “Kufungua Pazia” kinatumia simulizi halisi na mazingira ya kila siku kuelezea mantiki ya maendeleo nyuma ya Mpango wa 15 wa Miaka Mitano wa China. Kupitia simulizi za viwandani, watu na mambo halisi yaliyotokea, kinawapa watazamaji duniani mtazamo unaohusiana na kufikika zaidi kuhusu hatua inayofuata ya maendeleo ya China.
Katika sehemu ya nane ya “Kufungua Pazia,” Mina anawasili katika mji wa siku za baadaye baada ya kukusanya funguo zote saba za maendeleo, lakini anaishia kubaini tu kwamba mandhari zake za milima,bahari na mijini zimefifia na kuwa rangi ya kijivu.
Akitumai kurudisha rangi zao, Mina anazamia kwenye bahari ya kina akiwa na kifaa cha kuchunguza urejeshaji wa ikolojia, akiamini kuwa teknolojia ya hali ya juu inaweza kurejesha mfumo-ikolojia wa baharini kwa kubonyeza kitufe. Lakini baada ya kukutana na mhifadhi mwenyeji wa mazingira na kusikiliza simulizi zake kuhusu miaka mingi ya kazi za doria, utafiti na urejeshaji zilizofanywa na wafanyakazi wa kimazingira wa mstari wa mbele, Mina anaanza kuelewa kuwa urejeshaji wa ikolojia kamwe si mchakato wa kubonyeza kwa mara moja.
Teknolojia inaweza kufanya uhifadhi wa mazingira kuwa wenye usahihi na ufanisi zaidi, lakini haiwezi kuwa mbadala wa ustahimilivu, uwajibikaji na kujitolea kwa muda mrefu kwa binadamu. Mwishoni mwa sehemu hii, ukweli unadhihirishwa: ujumbe kutoka mwaka 2030 ambao umekuwa ukiongoza safari yake ulitumwa na Mina mwenyewe wa siku za baadaye.
Mwongozo wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030) unatoa wito wa azma isiyoyumbayumba kwa kanuni kuwa mito ya maji safi na milima ya kijani ni mali zenye thamani kubwa, na katika kuiweka kanuni hiyo katika vitendo halisi. Mpango huo ukiongozwa na lengo la kufika kilele cha utoaji kaboni na kufikia msawazisho wa utoaji kaboni, unahimiza juhudi kubwa zilizopangiliwa na kuratibiwa vema za kupunguza utoaji wa kaboni, kupunguza uchafuzi, kuelekea maendeleo ya kijani na kuongeza ukuaji wa uchumi, wakati huo huo kuimarisha nguzo za usalama wa ikolojia na kuimarisha vichocheo vya maendeleo ya kijani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



