Xi Jinping ampongeza Hichilema kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Zambia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 21, 2026

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amempongeza Hakainde Hichilema kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Zambia.

Kwenye salamu zake za pongezi za jana Alhamisi, Xi amesema kwamba wameshakutana mara mbili katika miaka ya hivi karibuni, na kwa pamoja wameongoza maendeleo ya uhusiano kati ya China na Zambia.“Kuaminiana kisiasa kati ya nchi zetu mbili kumeendelea kuongezeka kwa kina, ushirikiano wa kufuata hali halisi umepata matunda kemkem, na China na Zambia zimefanya uratibu na ushirikiano kwa karibu katika mambo ya pande nyingi," amesema.

Xi amesema ametilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Zambia, na yuko tayari kushirikiana na Hichilema ili kutekeleza matokeo ya Mkutano wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika.

Pia ameahidi kujiunga na kiongozi wa Zambia katika kuongeza urafiki wa jadi, kuimarisha hali ya kuungana mkono, na kuinua siku hadi siku kiwango cha ushirikiano wa kunufaishana, ili kuupeleka uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa China na Zambia kwenye kiwango kipya na kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha