Lugha Nyingine
Kampuni za China na Ethiopia zasaini mikataba yenye thamani ya dola milioni 330 za Marekani kwenye shughuli ya kutangaza biashara

Chen Hai, balozi wa China nchini Ethiopia, akizungumza kwenye Mkutano wa Ethiopia wa "Soko Kubwa kwa Wote: Mauzo ya Nje kwa China" mjini Addis Ababa, Ethiopia, Agosti 19, 2026. (Xinhua/Geng Xinning)
ADDIS ABABA - China imezindua Mkutano nchini Ethiopia unaoitwa "Soko Kubwa kwa Wote: Mauzo ya Nje kwa China" Jumatano wiki hii mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuhamasisha na kupanua mauzo ya nje ya bidhaa za Ethiopia kwenye soko la China.
Jumla ya mikataba 33 ya ushirikiano ilisainiwa kati ya kampuni za pande hizo mbili, yenye thamani ya jumla ya kimkataba ya dola zaidi ya milioni 330 za Marekani.
Akizungumza kwenye mkutanoi huo, Chen Hai, balozi wa China nchini Ethiopia, amesema mpango huo unalenga kulifanya soko kubwa la China kuwa soko la kuchangiwa duniani, kujenga ukuaji wa biashara wenye uwiano zaidi na kulinda mfumo wa biashara wa pande nyingi.
Chen amesema China inabaki kuwa mshirika mkubwa zaidi wa biashara na chanzo cha uwekezaji kwa Ethiopia, na inafungua soko lake kila mara kupitia kupanua utozaji wa sera za ushuru-sifuri, miongoni mwa mengine.
Kwa mujibu wa balozi huyo, mkutano huo ni udhihirisho wa msisitizo wa China katika kuongeza ushirikiano wake wa kiuchumi na biashara wa pande mbili na Ethiopia kupitia kuagiza bidhaa zenye viwango bora kutoka Ethiopia.
Kassahun Gofe, waziri wa biashara na mafungamano ya kikanda wa Ethiopia, amesema mauzo ya nje ya Ethiopia kwa China yalifikia dola za Marekani milioni 369 katika mwaka wa fedha wa Ethiopia wa 2025/2026 uliomalizika Julai 7, hali ambayo iliwakilisha ukuaji wa wastani wa asilimia 92 kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Amesema mpango huo wa "Soko Kubwa kwa Wote: Mauzo ya Nje kwa China" ni muhimu si tu katika kupanua mauzo ya kibiashara bali pia katika kusukuma mbele ushirikiano imara, wa kimkakati na wa kudumu kati ya China na Ethiopia.
Naye Chang Hui, naibu mkurugenzi mkuu wa Idara ya Biashara ya Nje katika Wizara ya Biashara ya China, ambaye aliongoza ujumbe wa kampuni za uagizaji nje bidhaa za China, amesema ushirikiano wa kimkakati wa hali zote kati ya China na Ethiopia umeendelea kuimarisha kwa kina ushirikiano wa kivitendo katika nyanja mbalimbali, na kutoa matokeo yenye matunda katika uhusiano wa kibiashara wa pande mbili.
Shughuli hiyo ya kutangaza biashara, iliyoandaliwa kwa ushirikiano na Wizara ya Biashara ya China, Ubalozi wa China nchini Ethiopia, Wizara ya Biashara na Mafungamano ya Kikanda ya Ethiopia, na Wizara ya Fedha ya Ethiopia, iliwaleta pamoja wawakilishi zaidi ya 200 wa China na Ethiopia wa biashara ya uagizaji-uuzaji nje, ambao wanatarajiwa kubadilishana taarifa za soko, kushiriki katika shughuli za kujenga ukaribu na kuanzisha na kupanua minyororo ya ugavi.

Wageni wakihudhuria Mkutano wa Ethiopia wa "Soko Kubwa kwa Wote: Mauzo ya Nje kwa China" mjini Addis Ababa, Ethiopia, Agosti 19, 2026. (Xinhua/Geng Xinning)

Wageni wakihudhuria Mkutano wa Ethiopia wa "Soko Kubwa kwa Wote: Mauzo ya Nje kwa China" mjini Addis Ababa, Ethiopia, Agosti 19, 2026. (Xinhua/Geng Xinning)

Kassahun Gofe, waziri wa biashara na mafungamano ya kikanda wa Ethiopia akizungumza kwenye Mkutano wa Ethiopia wa "Soko Kubwa kwa Wote: Mauzo ya Nje kwa China" mjini Addis Ababa, Ethiopia, Agosti 19, 2026. (Xinhua/Geng Xinning)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



