Lugha Nyingine
Serikali ya DRC na kundi la M23 wakubaliana juu ya mpangokazi kwa ajili ya mazungumzo ya amani
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kundi la waasi la M23 wamekubaliana juu ya mpangokazi kwa ajili ya mazungumzo ya amani, na kuweka bayana mlolongo wa hatua na muda maalum kwa mazungumzo ya siku za baadaye, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumamosi mwishoni mwa wiki iliyopita.
Pande hizo mbili zimesema kwamba, katika mazungumzo yaliyofanyika kuanzia tarehe 17 hadi 21 Agosti nchini Uswisi, zimetathmini hatua iliyopigwa na changamoto katika mchakato wa amani wa Doha, wakati huohuo zimejadili utekelezaji wa ahadi zilizopo na njia ya kuelekea mazungumzo chini ya Mfumokazi wa Makubaliano ya Doha.
Kufuatia tathmini hiyo, pande hizo mbili zimeandaa mpangokazi unaoweka bayana mlolongo wa hatua na ratiba kwa ajili ya mazungumzo ya siku zijazo. Pia zimekubaliana kuanzisha mfumo wa kufanya mapitio ya hatua iliyopigwa na kutatua changamoto katika utekelezaji wa wajibu na ahadi chini ya makubaliano ya mfumokazi huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



