Trump asaini amri kubadili jina la Ziwa Ontario kuwa "Ziwa Amerika" wakati kukiwa na mivutano ya kibiashara na Canada

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 28, 2026

WASHINGTON - Rais wa Marekani Donald Trump amesaini amri ya utendaji inayoagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo kubadilisha jina la Ziwa Ontario kuwa "Ziwa Amerika," ambapo mivutano ya kibiashara kati ya Marekani na Canada ikiendelea kupamba moto. "Tutabadilisha jina la Ziwa Ontario, mara moja, kuwa Ziwa Amerika," Trump amesema akiwa kwenye Ofisi ya Oval kabla ya kusaini amri hiyo jana Alhamisi. Hatua hiyo imekuja siku mbili tu baada ya Trump kusema kwenye mitandao ya kijamii kwamba Marekani inazingatia "kwa uzito" kubadilisha jina la Ziwa Ontario kuwa "Ziwa Amerika," akirejelea kwamba "hatutarajii kufanya tena biashara nyingi na Ontario." Ziwa Ontario, moja ya Maziwa Makuu matano ya Amerika Kaskazini, liko kwenye mpaka kati ya Marekani na Canada, huku jimbo la Canada la Ontario likiwa kaskazini na jimbo la New York la Marekani likiwa kusini. Jaribio hilo la Trump la kubadilisha jina la ziwa hilo linakuja wakati huu ambapo kuvunjika kwa mazungumzo ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili kumesababisha ushuru mpya wa kulipizana.  Marekani na Canada zilishindwa kufikia makubaliano ya kibiashara Agosti 21, na Marekani iliweka ushuru wa asilimia 50 kwa bidhaa za Canada zenye thamani ya dola takriban bilioni 20 za Marekani Agosti 22. Canada ilijibu kwa kutangaza ushuru wa kulipiza "dola kwa dola" kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani, ambao umepangwa kuanza kutumika Septemba 8. Maafisa wa Canada tayari wameshasema hawatatambua jina hilo jipya. Waziri wa Viwanda wa Canada Melanie Joly amesema kwamba Canada itaita kila mara eneo la maji hayo Ziwa Ontario. Amri hiyo ya utendaji ya hivi punde zaidi ni ya mara ya pili kwa Trump kupinga jina la muda mrefu la eneo la maji ya kimataifa na kiupande mmoja kulibadilisha jina kwa matumizi ya Marekani. Januari 20, 2025, siku ya kwanza ya muhula wake wa pili, Trump alisaini amri ya utendaji ya kubadilisha jina la Ghuba ya Mexico kuwa "Ghuba ya Amerika," hatua ambayo ilileta upingaji kutoka Mexico na wengine. Kwenye hafla hiyo ya Alhamisi ya kutia saini, Trump alisifu juhudi yake hiyo ya awali ya kubadilisha jina hilo la Ghuba ya Mexico. "Tuna ghuba na tuna ziwa. Sasa, tunachohitaji ni bahari. Kwa hiyo, labda tutalazimika kubadilisha jina la Atlantiki na/au Pasifiki. Labda tutazibadilisha zote mbili," Trump amesema.

Picha hii iliyopigwa Januari 21, 2025 ikionyesha Ziwa Ontario lililoganda, Toronto, Canada. (Picha na Zou Zheng/Xinhua)

WASHINGTON - Rais wa Marekani Donald Trump amesaini amri ya utendaji inayoagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo kubadilisha jina la Ziwa Ontario kuwa "Ziwa Amerika," ambapo mivutano ya kibiashara kati ya Marekani na Canada ikiendelea kupamba moto.

"Tutabadilisha jina la Ziwa Ontario, mara moja, kuwa Ziwa Amerika," Trump amesema akiwa kwenye Ofisi ya Oval kabla ya kusaini amri hiyo jana Alhamisi.

Hatua hiyo imekuja siku mbili tu baada ya Trump kusema kwenye mitandao ya kijamii kwamba Marekani inazingatia "kwa uzito" kubadilisha jina la Ziwa Ontario kuwa "Ziwa Amerika," akirejelea kwamba "hatutarajii kufanya tena biashara nyingi na Ontario."

Ziwa Ontario, moja ya Maziwa Makuu matano ya Amerika Kaskazini, liko kwenye mpaka kati ya Marekani na Canada, huku jimbo la Canada la Ontario likiwa kaskazini na jimbo la New York la Marekani likiwa kusini.

Jaribio hilo la Trump la kubadilisha jina la ziwa hilo linakuja wakati huu ambapo kuvunjika kwa mazungumzo ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili kumesababisha ushuru mpya wa kulipizana.

Marekani na Canada zilishindwa kufikia makubaliano ya kibiashara Agosti 21, na Marekani iliweka ushuru wa asilimia 50 kwa bidhaa za Canada zenye thamani ya dola takriban bilioni 20 za Marekani Agosti 22.

Canada ilijibu kwa kutangaza ushuru wa kulipiza "dola kwa dola" kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani, ambao umepangwa kuanza kutumika Septemba 8.

Maafisa wa Canada tayari wameshasema hawatatambua jina hilo jipya. Waziri wa Viwanda wa Canada Melanie Joly amesema kwamba Canada itaita kila mara eneo la maji hayo Ziwa Ontario.

Amri hiyo ya utendaji ya hivi punde zaidi ni ya mara ya pili kwa Trump kupinga jina la muda mrefu la eneo la maji ya kimataifa na kiupande mmoja kulibadilisha jina kwa matumizi ya Marekani.

Januari 20, 2025, siku ya kwanza ya muhula wake wa pili, Trump alisaini amri ya utendaji ya kubadilisha jina la Ghuba ya Mexico kuwa "Ghuba ya Amerika," hatua ambayo ilileta upingaji kutoka Mexico na wengine.

Kwenye hafla hiyo ya Alhamisi ya kutia saini, Trump alisifu juhudi yake hiyo ya awali ya kubadilisha jina hilo la Ghuba ya Mexico.

"Tuna ghuba na tuna ziwa. Sasa, tunachohitaji ni bahari. Kwa hiyo, labda tutalazimika kubadilisha jina la Atlantiki na/au Pasifiki. Labda tutazibadilisha zote mbili," Trump amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha