Lugha Nyingine
Waziri wa Afya wa DRC aipongeza China kwa kuiita kuwa ni mshirika wa afya wa kipaumbele

Roger Kamba (kushoto), Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), akihudhuria hafla ya makabidhiano ya msaada wa dharura wa kibinadamu wa China kwa DRC huko Kinshasa, DRC, Agosti 26, 2026. (Xinhua)
China kwa muda mrefu imekuwa ikiunga mkono maendeleo ya sekta ya afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na inabaki kuwa mshirika muhimu na wa kipaumbele, amesema Waziri wa Afya wa DRC Roger Kamba.
Kamba ameyasema hayo siku ya Jumatano wiki hii kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Kinshasa kwa ajili ya msaada wa dharura wa kibinadamu wa China kwa DRC. Balozi wa China nchini DRC Zhao Bin na Kamba walitia saini kwenye hati za makabidhiano za miradi mitatu ya msaada kwenye hafla hiyo.
Kamba amesema, China iliitikia kwa haraka baada ya mlipuko mpya wa Ebola kutangazwa nchini DRC mwezi wa Mei, ikitoa msaada wa dharura katika hatua ya mapema na kutuma kwa mfululizo makundi matatu ya wataalamu wa matibabu ili kuunga mkono mwitikio wa nchi hiyo kwa mlipuko huo.
Vitu na fedha za kukabiliana na maambukizi vilivyotolewa na China tayari vimeshaanza kutumiwa kwenye mistari ya mbele ya kukabiliana na janga hilo, na vimetoa uungaji mkono imara kwa juhudi za DRC za kudhibiti mlipuko, amesema.
China imekuwa ikitoa uungaji mkono usiokoma kwa maendeleo ya sekta ya afya ya DRC kwa miaka mingi na inaendelea kuwa mshirika muhimu na wa kipaumbele katika sekta hiyo, amesema Kamba.
Kwa upande wake Zhao amesema ushirikiano wa afya wa China na DRC una msingi imara na unaunda sehemu muhimu ya ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili.
Katika kukabiliana na mlipuko wa sasa wa Ebola, China ilichukua hatua kwa haraka ili kutoa msaada wa dharura wa kibinadamu na ilituma makundi matatu mfululizo ya wataalamu wa matibabu katika DRC, kuunga mkono mwitikio wa nchi hiyo wa kukabiliana na mlipuko na juhudi za kulinda afya ya watu kwa kupitia hatua madhubuti, amesema Zhao.
Uungaji mkono wa namna hiyo unaakisi urafiki wa kina kati ya watu wa China na DRC, ambao wamekuwa wakisimama pamoja na kusaidiana katika nyakati za mambo magumu, ameongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



