Lugha Nyingine
Xi aanza ziara ya kiserikali nchini Kyrgyzstan, asifu "kipindi cha dhahabu" cha ushirikiano

Rais wa China Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan wakitoka nje ya ndege baada ya kuwasili Bishkek, Kyrgyzstan, Agosti 30, 2026. (Xinhua/Zhai Jianlan)
BISHKEK - Rais wa China Xi Jinping amefika Bishkek, Kyrgyzstan jana Jumapili kwa ziara ya kiserikali nchini Kyrgyzstan na Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) 2026 ambapo katika hotuba yake ya maandishi iliyotolewa mara baada ya kuwasili huko amesema ushirikiano kati ya China na Kyrgyzstan umeingia kwenye "kipindi cha dhahabu" cha maendeleo ya haraka.
Akisema kuwa China na Kyrgyzstan zimekuwa na urafiki wa jadi wa muda mrefu, na Milima mirefu ya Tianshan inayosimama kidete kama mashuhuda wa mawasiliano ya kirafiki kati ya watu wa nchi mbili katika miaka elfu moja iliyopita. Amesema katika miaka 34 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, uhusiano kati ya China na Kyrgyzstan umejaribiwa katika mabadiliko ya mazingira ya kimataifa, siku zote umedumisha maendeleo mazuri na tulivu, na kufikia kiwango cha juu ya uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote katika zama mpya.
Xi amesema kwamba wakati wa ziara hiyo atabadilishana maoni kwa kina na Rais wa Kyrgyzstan Sadyr Japarov kuhusu uhusiano kati ya China na Kyrgyzstan, ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya nchi hizo mbili, na masuala ya kimataifa na kikanda yanayofuatiliwa kwa pamoja, na kuweka dira mpya kwa ajili ya kujenga jumuiya ya China na Kyrgyzstan yenye mustakabali wa pamoja.
"Ninatarajia kuhudhuria Mkutano wa SCO Bishkek, kukumbuka pamoja na pande zote kuhusu uzoefu wa miaka 25 wa maendeleo ya SCO, kwa pamoja kujadili mipango ya ushirikiano, kujenga mustakabali wa jumuiya, na kuhimiza maendeleo mapya endelevu ya SCO," Xi amesema.
Kabla ya ziara yake ya kiserikali nchini Kyrgyzstan na kuhudhuria mkutano huo wa viongozi wa SCO, Xi siku ya Ijumaa alichapisha makala iliyosainiwa naye yenye kichwa "Kuanzisha kwa Pamoja Hali Mpya ya Maendeleo Yenye Sifa Bora ya Uhusiano kati ya China na Kyrgyzstan" kwenye Gazeti la Serikali la Slovo Kyrgyzstan na Shirika la Habari la Kitaifa la Kabar.
Akieleza kuwa hiyo itakuwa ziara yake ya tatu katika nchi hiyo nzuri, na anatarajia kushirikiana na Rais Japarov katika kuweka dira mpya kwa ajili ya uhusiano kati ya China na Kyrgyzstan na kupiga hatua mpya katika kujenga jumuiya ya SCO yenye mustakabali wa pamoja.
Katika makala hiyo, Xi pia ametoa wito kwa pande hizo mbili kuimarisha ujirani mwema na urafiki, kutafuta kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja, kuenzi urafiki wa jadi, na kutekeleza ushirikiano wa pande nyingi.

Rais wa China Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan wakitoka nje ya ndege baada ya kuwasili Bishkek, Kyrgyzstan, Agosti 30, 2026. (Xinhua/Wang Ye)

Rais wa China Xi Jinping akiwasili Bishkek kwa kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) 2026 na kufanya ziara ya kiserikali nchini Kyrgyzstan kutokana na mwaliko wa Rais Sadyr Japarov wa Kyrgyzstan, Agosti 30, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais wa China Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan, pamoja na Rais wa Kyrgyz Sadyr Japarov na mkewe Aigul Japarova, kwa pamoja wakifurahia kusikiliza nyimbo za Kichina zilizokuwa zikiimbwa na vijana wa Bishkek, Kyrgyzstan, Agosti 30, 2026. (Xinhua/Yan Yan)

Rais wa China Xi Jinping akiwasili Bishkek kwa kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) 2026 na kufanya ziara ya kiserikali nchini Kyrgyzstan kutokana na mwaliko wa Rais Sadyr Japarov wa Kyrgyzstan, Agosti 30, 2026. (Xinhua/Ding Lin)

Rais wa China Xi Jinping akiwasili Bishkek kwa kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) 2026 na kufanya ziara ya kiserikali nchini Kyrgyzstan kutokana na mwaliko wa Rais Sadyr Japarov wa Kyrgyzstan, Agosti 30, 2026. (Xinhua/Li Renzi)

Rais wa China Xi Jinping akiwasili Bishkek kwa kuhudhuria kweynye Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) 2026 na kufanya ziara ya kiserikali nchini Kyrgyzstan kutokana na mwaliko wa Rais Sadyr Japarov wa Kyrgyzstan, Agosti 30, 2026. (Xinhua/Wang Ye)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



