Xi atarajia uhusiano wa China na Russia uwe na msingi imara zaidi na mustakabali mzuri zaidi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 01, 2026

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Russia Vladimir Putin katika wakati wa Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai 2026, huko Bishkek, Kyrgyzstan, Agosti 31, 2026. (Xinhua/Li Xiang)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Russia Vladimir Putin katika wakati wa Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai 2026, huko Bishkek, Kyrgyzstan, Agosti 31, 2026. (Xinhua/Li Xiang)

BISHKEK - Rais wa China Xi Jinping amesema kwamba, chini ya uelekezaji wa kimkakati wake na wa Rais wa Russia Vladimir Putin na kupitia juhudi za pamoja za pande zote mbili, msingi wa uhusiano kati ya China na Russia utakuwa wa imara zaidi, maendeleo yake yatakuwa kwa hatua madhubuti zaidi, na mustakabali wao utakuwa mzuri zaidi.

Xi ameyasema hayo jana Jumatatu kwenye mkutano na Putin katika wakati wa Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) 2026 mjini Bishkek, Kyrgyzstan.

Amesema kwamba wakati wa ziara ya kiserikali ya Putin yenye mafanikio nchini China mwezi Mei, yeye na Putin walifanya mipango ya kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa pande mbili kuelekea ya sifa bora zaidi na ya kiwango cha juu zaidi kutoka kwa mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu, na walifikia maoni ya pamoja kuhusu kuzidisha ushirikiano kati ya China na Russia katika sekta mbalimbali katika hali mpya ya kimataifa.

"Mamlaka husika za nchi zetu mbili zinafanya juhudi za kutekeleza maoni hayo ya pamoja, na matokeo halisi yamepatikana," Xi amesema, akiongeza kuwa mawasiliano na ushirikiano kati ya pande hizo mbili yamedumisha mwelekeo wenye nguvu.

Xi ameeleza kuwa hali ya kimataifa isiyo na uhakika na isiyoweza kukadiriwa zinaongezeka kidhahiri katika wakati wa kuhimizwa kwa kasi kwa mabadiliko makubwa ambayo hayajawahi kuonekana katika miaka mia moja iliyopita. "Lakini watu wa nchi mbalimbali duniani bado hawajabadilisha utafutaji wao juu ya amani, maendeleo, ushirikiano wa kunufaishana na matokeo mazuri kwa pamoja."

Amesema SCO inabeba wajibu muhimu kwa ajili ya kulinda utulivu wa kikanda na kuhimiza maendeleo ya kikanda.

Kwa upande wake Putin amesema katikati ya mazingira ya kimataifa yenye misukosuko na utatanishi, Russia na China zimezidisha bila kusita uratibu wao wa kimkakati wa pande zote, kushikilia usawa, kuaminiana, na kuungana mkono, wakati ushirikiano na maendeleo katika sekta mbalimbali vimesukumwa mbele kwa kasi, na uhusiano kati ya Russia na China umekuwa mfano wa kuigwa kwa uhusiano kati ya nchi na nchi.

"Russia inapenda kudumisha mawasiliano na China kwenye ngazi ya juu, kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara, nishati, viwanda, usafirishaji, na sayansi na teknolojia, kuongeza mawasiliano kati ya watu na ya kitamaduni, na kuhimiza uhusiano wa pande mbili ufikie matokeo mapya," amesema.

Amesema Russia inapenda kuimarisha uratibu na ushirikiano na China ndani ya mifumo ya pande nyingi kama vile Umoja wa Mataifa, mfumo wa BRICS na wa G20, kuiunga mkono China katika kuandaa Mkutano wa Viongozi wa Uchumi wa APEC, na kwa pamoja kulinda amani, utulivu na ustawi duniani.

Marais hao wawili wa nchi pia wamebadilishana maoni juu ya masuala ya kimataifa na kikanda yanayofuatiliwa kwa pamoja.

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Russia Vladimir Putin  katika wakati wa Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai 2026, Bishkek, Kyrgyzstan, Agosti 31, 2026. (Xinhua/Yan Yan)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Russia Vladimir Putin katika wakati wa Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai 2026, Bishkek, Kyrgyzstan, Agosti 31, 2026. (Xinhua/Yan Yan)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha