Lugha Nyingine
Xi na Japarov wapanga mwelekeo mpya kwa uhusiano kati ya China na Kyrgyzstan

Rais wa China Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan wakipiga picha ya kundi na Rais wa Kyrgyzstan Sadyr Japarov na mkewe Aigul Japarov huko Bishkek, Kyrgyzstan, Agosti 31, 2026. Xi alifanya mazungumzo na Japarov huko siku ya Jumatatu. (Xinhua/Yan Yan)
Rais Xi Jinping amesema huko Bishkek kuwa China ipo tayari kufanya kazi pamoja na Kyrgyzstan ili kuleta matunda mengi zaidi ya kivitendo ya ushirikiano ambayo ni halisi na yenye kufikika.
Xi ameyasema hayo jana Jumatatu kwenye mazungumzo na Rais wa Kyrgyzstan Sadyr Japarov. Xi aliwasili Bishkek Jumapili kwa ajili ya ziara ya kiserikali nchini Kyrgyzstan na kushiriki kwenye mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) 2026.
Ziara yake hiyo imekuja wakati ambapo ushirikiano wa China na Kyrgyzstan ukiwa umeingia kwenye “kipindi cha dhahabu” cha maendeleo ya kasi, kama ilivyoelezwa na Xi katika hotuba ya maandishi iliyotolewa alipowasili, huku nchi hizo mbili zikifanya kazi kwa pamoja kubadilisha urafiki wao wa muda mrefu na kuaminiana imara kisiasa kuwa ushirikiano mpana zaidi na manufaa makubwa zaidi kwa watu wao.
Ziara hiyo inakutana na maadhimisho ya miaka 35 ya uhuru wa Kyrgyzstan. Kwa niaba ya serikali ya China na watu wake, Xi kwanza aliwasilisha pongezi kwa Japarov kwa tukio hilo la Siku ya Uhuru ya Kyrgyzstan.
Xi amesema katika miaka ya hivi karibu, uhusiano kati ya China na Kyrgyzstan umepata maendeleo ya hatua kubwa chini ya mwongozo wa pamoja wa viongozi hao wawili, huku ushirikiano kwenye nyanja mbalimbali ukistawi, hali ambayo imechochea maendeleo ya pande zote mbili na kuleta manufaa kwa watu wao, wakati huohuo ikichangia amani, utulivu na ustawi katika kanda.
Kwa upande wake, Japarov amesema Kyrgyzstan na China ni nchi jirani, na Njia ya kale ya Hariri imeziunganisha kwa karibu. Amesema, katika miaka ya hivi karibuni, huku kukiwa na maendeleo ya kasi ya uhusiano wa washirika wa kimkakati wa pande zote wa Kyrgyzstan na China kwa zama mpya, uhusiano wa pande mbili umeingia kwenye hatua ya dhahabu na kufikia kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa katika historia.
Baada ya mazungumzo yao hayo, viongozi hao wawili walitia saini kwenye taarifa ya pamoja ya Jamhuri ya Watu wa China na Jamhuri ya Kyrgyz juu ya maendeleo yenye sifa bora ya uhusiano wa washirika wa kimkakati wa pande zote kwa zama mpya, na mkataba wa pande mbili juu ya ujirani, urafiki na ushirikiano mzuri wa kudumu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



