Xi Jinping atoa pendekezo la pointi-nne kwenye mkutano wa viongozi wa SCO wa Bishkek

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 02, 2026

Rais wa China Xi Jinping akitoa hotuba muhimu kwenye Mkutano wa 26 wa Baraza la Wakuu wa Nchi la Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO), huko Bishkek, Kyrgyzstan, Septemba 1, 2026. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Rais wa China Xi Jinping akitoa hotuba muhimu kwenye Mkutano wa 26 wa Baraza la Wakuu wa Nchi la Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO), huko Bishkek, Kyrgyzstan, Septemba 1, 2026. (Xinhua/Zhai Jianlan)

BISHKEK - Rais wa China Xi Jinping ametoa pendekezo la pointi-nne kwenye Mkutano wa 26 wa Baraza la Wakuu wa Nchi la Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) huko Bishkek, mji mkuu wa Kyrgyzstan.

Katika hotuba yake kwenye mkutano huo jana Jumanne, Xi alisema mwaka huu ni wa maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa SCO. Amesema katika miaka 25 iliyopita, kulinda mamlaka ya nchi, usalama na maslahi ya maendeleo kumekuwa maoni ya pamoja ya nchi za kanda hii katika wakati wa kukabiliwa na mafunzo makubwa ya Vita vya Baridi, tishio halisi linaloletwa na "nguvu tatu ovu," pamoja na matarajio makubwa ya watu wa nchi mbalimbali juu ya amani na maendeleo.

"Hivyo jumuiya ya SCO ilianzishwa wakati huo, na jumuiya hii imeonesha nguvu hai kubwa zaidi siku hadi siku,” Xi ameongeza.

Xi amesema katika miaka 25 iliyopita, SCO imepitia safari isiyo ya kawaida. Amesema kuwa mafanikio yake muhimu zaidi yamekuwa ni kwamba jumuiya hiyo inabadilika hatua kwa hatua hadi kuwa jumuiya ya ushirikiano wa kikanda ya aina mpya, ambayo inahusisha eneo kubwa zaidi la kijiografia, idadi kubwa zaidi ya watu, na kuwa jumuiya yenye nguvu kubwa ya kujiendeleza duniani.

"Mali muhimu zaidi ya kutia moyo ya SCO ni pendekezo la mwanzo kabisa na kufuata kithabiti 'Moyo wa Shanghai' ulio wa kuaminiana, kunufaishana, kuwa na usawa, mashauriano, kuheshimu ustaarabu mbalimbali na kutafuta maendeleo kwa pamoja,” amesema.

Xi amesema kuwa miaka 25 imepita, kadri mabadiliko makubwa ambayo hayakutokea katika miaka mia moja iliyopita yanavyozidi kuongezeka kwa kasi, ndivyo ushindani unavyozidi kuongezeka katika wakati wa kufanya mazungumzo na mapambano, ushirikiano wa kunufaishana au kutiana hasara, na ushirikiano wa pande nyingi na ule wa upande mmoja, na kivuli cha vita kingali bado kinasumbua dunia.

"Katika njia panda kuhusu mustakabali wa binadamu, SCO inapaswa kubeba wajibu wake wa kihistoria na kuchukua hatua katika kuongoza mchakato wa historia," amesema.

Xi ametoa wito kwa SCO kuipa kipaumbele kazi ya kujiendeleza, na kuanzisha pamoja siku za baadaye zenye ustawi kwa pamoja.

Xi amehimiza jumuiya ya SCO kushikilia kuchukua usalama kuwa lengo muhimu, na kujenga mazingira ya usalama kwa pamoja.

Xi pia ametoa wito wa kuitaka jumuiya hiyo kuwaweka wananchi kwenye nafasi ya kwanza, na kuimarisha msingi wa urafiki wa milele.

Xi pia ameihimiza SCO kusukuma mbele mazungumzo na mashauriano, na kujitahidi kufikia usimamizi wenye usawa na utaratibu zaidi.

Mkutano huo pia umeamua kwamba Pakistan itakuwa nchi mwenyekiti wa zamu wa SCO kwa mwaka 2026-2027.

Rais wa China Xi Jinping akisalimiana na Rais wa Kyrgyz Sadyr Japarov huko Bishkek, Kyrgyzstan, Septemba 1, 2026. (Xinhua/Wang Ye)

Rais wa China Xi Jinping akisalimiana na Rais wa Kyrgyz Sadyr Japarov huko Bishkek, Kyrgyzstan, Septemba 1, 2026. (Xinhua/Wang Ye)

Rais wa China Xi Jinping akipiga picha pamoja na viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO), Bishkek, Kyrgyzstan, Septemba 1, 2026. (Xinhua/Wang Ye)

Rais wa China Xi Jinping akipiga picha pamoja na viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO), Bishkek, Kyrgyzstan, Septemba 1, 2026. (Xinhua/Wang Ye)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha