Lugha Nyingine
Zanzibar yawatunuku timu ya madaktari na wataalamu wa kichocho wa China kwa mchango wa huduma ya afya

Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikimwonesha Kaimu Waziri wa Afya wa Zanzibar Saada Mkuya Salum (wa pili, kulia) akikabidhi cheti cha heshima kwa kundi la tatu la wataalamu chini ya awamu ya pili ya mradi wa kuzuia na kudhibiti kichocho unaosaidiwa na China, visiwani Zanzibar, Tanzania, Agosti 31, 2026. (Timu ya Wataalamu wa Mradi wa Kuzuia na Kudhibiti Kichocho unaosaidiwa na China/kupitia Xinhua)
DAR ES SALAAM - Wizara ya Afya ya Tanzania Zanzibar imewapongeza Kundi la 35 la timu ya madaktari wa China visiwani Zanzibar na kundi la tatu la wataalamu chini ya awamu ya pili ya mradi wa kuzuia na kudhibiti kichocho unaosaidiwa na China kwa mchango wao kwa sekta ya afya ya visiwa hivyo.
Kwenye hafla iliyofanyika Jumatatu wiki hii, Kaimu Waziri wa Afya wa Zanzibar Saada Mkuya Salum amewapongeza wataalamu hao wa matibabu na afya wa China kwa kutoa rasilimali za matibabu zenye ubora wa hali ya juu na utaalamu wa kitaalamu wakati wakitekeleza usaidizi wa kimatibabu na mipango ya kuzuia na kudhibiti kichocho kulingana na mahitaji ya ndani.
Amesema ushirikiano huo umeleta manufaa halisi kwa jamii za ndani na umeonyesha urafiki wa muda mrefu na ushirikiano wa kivitendo kati ya Tanzania na China.
Bao Zengtao, kiongozi wa timu hiyo ya matibabu ya China, amesema timu za matibabu za China zitaendelea kuzidisha ubadilishanaji katika matibabu, mafunzo ya kiufundi na ushirikiano wa afya ya umma na Zanzibar katika siku zijazo.
Wang Wei, mkuu wa timu hiyo ya wataalamu wa kuzuia na kudhibiti kichocho, ameeleza matumaini yake kwamba pande hizo mbili zitaimarisha zaidi ushirikiano ili kuimarisha na kupanua mafanikio katika kuzuia kichocho visiwani Zanzibar.
Kundi hilo la 35 la timu ya madaktari wa China liliwasili Zanzibar mwezi Septemba mwaka jana na limetibu wagonjwa wasiolazwa karibu 60,000 wakati wa kipindi chake. Awamu ya pili ya mradi wa kuzuia na kudhibiti kichocho unaosaidiwa na China ilizinduliwa Septemba 2023 na kukamilisha kukubalika kwake kwenye eneo lake la mradi mwezi Agosti 2026.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



