Mkoa wa Xinjiang, China wasukuma mbele maendeleo na matumizi ya nishati (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 03, 2026
Mkoa wa Xinjiang, China wasukuma mbele maendeleo na matumizi ya nishati
Mfanyakazi akifanya jaribio la kuiga uhalisia kwenye Kampuni ya Maendeleo ya Teknolojia Mpya ya Xinjiang Keli, Karamay, Mkoa Unaojiendesha wa Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China, Septemba 1, 2026. (Xinhua/Ding Lei)

Katika Mwaka huu wa 2026, ambao ni mwaka wa kwanza wa kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano wa China, Mkoa Unaojiendesha wa Xinjiang umeendelea kubeba kithabiti majukumu yake ya kimkakati na kuharakisha mpito kuelekea maendeleo na matumizi ya nishati yaliyo ya kijani, janja na fanisi zaidi.

Katika sekta ya mafuta na gesi, mfululizo wa teknolojia kuu muhimu zimeshuhudia mafanikio makubwa, hali ambayo imeufanya mkoa huo kufikia maendeleo yenye faida kiuchumi ya rasilimali zisizo za kawaida za mafuta na gesi wakati huohuo ukiongeza kwa kiasi kikubwa tija kwenye kisima kimoja.

Wakati huo huo, miradi mipya zaidi ya nishati inayochanganya uzalishaji umeme kwa jua na uhifadhi nishati wa muda mrefu inasaidia kutoa nishati safi kwa makumi ya maelfu ya kaya. Teknolojia za kidijitali na za AI zimekuwa zikitumika katika mchakato mzima wa uchimbaji, maendeleo na uzalishaji wa nishati.

Mkoa huo wa Xinjiang unatumia sifa zake bora za rasilimali wakati huohuo ukiwezesha uvumbuzi kuchukua jukumu kubwa zaidi katika juhudi zisizokoma za kuweka msingi imara kwa mfumo wa kisasa wa viwanda.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha