Mashindano ya kuchagua vipaji kwa ajili ya Maonesho ya "Imba kwa Afrika" yafanyika Kenya (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 07, 2026
Mashindano ya kuchagua vipaji kwa ajili ya Maonesho ya
Mwanamke akishiriki kwenye mashindano ya msimu wa pili ya kuchagua vipaji vya muziki kwa ajili ya maonesho ya "Imba kwa Afrika", Kibera, Nairobi, Kenya, Septemba 5, 2026. (Xinhua/Xie Jianfei)

Mashindano ya msimu wa pili ya kuchagua vipaji vya maonesho ya "Imba kwa Afrika" ambayo ni moja ya miradi mikuu ya Mwaka 2026 wa Mawasiliano Kati ya Watu wa China na Afrika yamefanyika katika eneo la Kibera, jijini Nairobi, Kenya siku ya Jumamosi.

Mashindano hayo ya kuchagua vipaji vya muziki kwa ajili ya maonesho ya "Imba kwa Afrika" yanayoungwa mkono na China yanalenga kuwaandaa vipaji vya muziki nchini Kenya, wakati huohuo kujenga jukwaa kwa ajili ya kuhimiza mazungumzo ya kuvuka-tamaduni.

Msimu wa pili wa mashindano ya kuchagua vipaji vya muziki yanashirikisha safu ya wanawake pekee, ukiandaaliwa kwenye msingi wa mafanikio ya msimu wa kwanza ambao ulishirikisha washindani wa kiume pekee ulioanza Novemba 2025 hadi Februari mwaka huu.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha