Matufaha ya kuiva mapema katika Mkoa wa Guizhou, China yaingia msimu wa mavuno (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 07, 2026
Matufaha ya kuiva mapema katika Mkoa wa Guizhou, China yaingia msimu wa mavuno
Wafanyakazi wakibeba matufaha yaliyopangiliwa kwenye kiwanda cha matunda katika Wilaya Inayojiendesha ya Makabila ya Wayi na Wamiao ya Weining, Bijie, Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China, Septemba 5, 2026. (Xinhua/Tao Liang)

Matufaha ya kuiva mapema katika Wilaya Inayojiendesha ya Makabila ya Wayi na Wamiao ya Weining, Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China siku hadi siku yanaingia msimu wa mavuno. Kaitka wilaya hiyo kumekuwa na mashamba ya hekta karibu 10,000 ya miti ya matufaha inayozaa matunda, na matufaha ya miti hiyo yamefikia aina zaidi ya kumi.

Shughuli za matufaha za wilaya hiyo zimeleta mapato ya thamani ya jumla ya yuan bilioni 1.2 (dola karibu milioni 178.81 za Marekani), hali ambayo imeongeza mapato ya familia za wakulima karibu 100,000 za vijijini.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha