China na Laos zatumia droni na roboti za umbo la mbwa kwenye mazoezi ya kimatibabu ya “Peace Train-2026"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 11, 2026
China na Laos zatumia droni na roboti za umbo la mbwa kwenye mazoezi ya kimatibabu ya “Peace Train-2026
Wajumbe wa timu shiriki wakitumia mifumo ya uokoaji inayoendeshwa kwa mbali na kiotomatiki bila binadamu ndani yake kwenye awamu ya mafunzo ya pamoja ya vitengo-mchanganyiko ya mazoezi ya pamoja ya uokoaji wa kimatibabu wa kibinadamu ya "Peace Train-2026" ya China-Laos, Vientiane, Laos, Septemba 9, 2026. (Picha na Zeng Li/Xinhua)

VIENTIANE – Droni za utafutaji na uokoaji zimepaa angani kwa ajili ya upelelezi wa angani wa eneo kubwa, roboti za umbo la mbwa zenye miguu minne zimekaribia maeneo ya maafa ili kulifanyia uchambuzi eneo la tukio, na magari malori yanayojiendesha bila dreva yamesonga mbele kusafirisha "majeruhi" – Hayo yote yalionekana jana Jumatano kwenye mazoezi ya pamoja ya uokoaji wa kimatibabu wa kibinadamu ya "Peace Train-2026" ya China-Laos yanayoendelea hivi sasa katika mji mkuu wa Laos, Vientiane.

Jumatano wiki hii, mazoezi hayo ya pamoja ya kijeshi ya China-Laos yaliingia katika awamu ya mafunzo ya pamoja ya vitengo-mchanganyiko.

Kwa mara ya kwanza, vifaa vya AI vinavyoendeshwa kwa mbali na kiotomatiki bila binadamu ndani yake vilitumika kwa mpangilio mzuri kufanya utafutaji na uokoaji wa majeruhi kwa wakati mmoja, uokoaji na usafirishaji, na usambazaji wa vifaa. Ujumuishaji wa vifaa vinavyoendeshwa kwa mbali bila dereva umeboresha mfumo wa uokoaji wa kimatibabu katika uwanja wa mafunzo.

Xu Chao, mjumbe wa timu shiriki, ameelezea kwamba mafunzo hayo yalizingatia falsafa ya "kumtilila maanani binadamu" wakati huohuo yametumia vifaa vinavyoendeshwa kwa mbali na kiotomatiki bila binadamu ndani yake ili kuongeza uwezo.

Amesema mifumo inayoendeshwa kwa mbali na kiotomatiki bila binadamu ndani yake imetumika katika mchakato mzima wa uokoaji na matibabu, kuanzia utafutaji na uokoaji wa majeruhi kwenye mstari wa mbele na uwasilishaji kwa usahihi wa vifaa vya dharura hadi uhamishaji kwa haraka wa majeruhi na matibabu yanayofuatia baadaye kwenye vituo vya matibabu vya nyuma.

Xu amebainisha kuwa vifaa hivyo vinavyoendeshwa kwa mbali na kiotomatiki bila binadamu ndani yake, zikiwemo droni, roboti za umbo la mbwa, na magari yanayojiendesha yenyewe bila dereva, vinaweza kuingia katika maeneo hatari ili kutekeleza majukumu ya utafutaji na uokoaji, na kusaidia wafanyakazi kuitikia kwa haraka na kwa ufanisi zaidi.

"Mifumo hii imeundwa ili kukidhi mahitaji ya kazi ngumu, kuboresha ufanisi wa utafutaji na uokoaji wa majeruhi na uhamishaji watu wa masafa marefu, na kuongeza uharaka wa muda wa shughuli za utafutaji na uokoaji na uhamishaji watu kupitia kubaini kwa wakati halisi na mwitikio wa haraka," ameongeza.

"Mafunzo haya ya kutumia vifaa vinavyoendeshwa kwa mbali na kiotomatiki bila binadamu ndani yake vinawakilisha hatua ya mabadiliko makubwa katika matumizi jumuishi ya vikosi vya uokoaji wa kimatibabu vinavyoendeshwa kwa mbali na kiotomatiki bila binadamu ndani yake," amesema Chen Peizheng, afisa wa mazoezi hayo wa China. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha