Waziri wa Ulinzi wa China asema China iko tayari kuchangia uzoefu wa ujenzi wa jeshi wakati PLA ikikaribia kutimiza miaka 100

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 17, 2026

Picha hii iliyopigwa tarehe 16 Septemba 2026 inaonyesha  hali ya ufunguzi wa Jukwaa la 13 la Xiangshang la Beijing, nchini China. (Picha na Han Qiyang/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa tarehe 16 Septemba 2026 inaonyesha hali ya ufunguzi wa Jukwaa la 13 la Xiangshang la Beijing, nchini China. (Picha na Han Qiyang/Xinhua)

Waziri wa Ulinzi wa China Bw. Dong Jun amesema jeshi la China liko tayari kubadilishana uzoefu wake katika kujenga vikosi vya kijeshi wakati Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) linapokaribia kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake.

Akiongea kwenye ufunguzi wa Jukwaa la 13 la Xiangshan la Beijing, Bw. Dong amesema "Wakati jeshi la China linakaribia kuadhimisha miaka 100, tunaongeza kasi ya ujenzi wetu wa mambo ya kisasa. Tuko tayari kubadilishana uzoefu na mawazo yetu na pande mbalimbali kuhusu kujenga na kusimamia vikosi vya jeshi."

Bw. Dong ameongeza kuwa jeshi la China pia linapenda kutoa msaada kwa nchi zinazohitaji msaada kadiri ya uwezo wake.

Jeshi la PLA lilianzishwa wakati wa Uasi wa Nanchang Agosti 1, 1927, ulioashiria mwanzo wa uongozi wa kujiamulia wa Chama cha Kikomunisti cha China katika vita vya mapinduzi.

Bw. Dong pia amesema kwenye kukabiliana na majanga ya asili ya ghafla na ya mara kwa mara, jeshi la China limekuwa tayari kufanya kila liwezalo na kutoa msaada pale inapohitajika.

Picha hii iliyopigwa tarehe 16 Septemba 2026 inaonyesha ufunguzi wa Jukwaa la 13 la Xiangshan la Beijing nchini China. (Picha na Han Qiyang/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa tarehe 16 Septemba 2026 inaonyesha ufunguzi wa Jukwaa la 13 la Xiangshan la Beijing nchini China. (Picha na Han Qiyang/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha