Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China: SCO yapaswa kuhimiza utulivu na ustawi wa kikanda, na kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya dunia

Tarehe 20 Oktoba 2026, Waziri Mkuu wa Baraza la Serikali la China Li Qiang akihudhuria kwenye Mkutano wa 25 wa Baraza la Wakuu wa Serikali (Waziri Mkuu) wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) huko Dushanbe, Tajikistan. (Xinhua/Shen Hong)
Waziri Mkuu wa Baraza la Serikali la China Li Qiang jana Jumanne alisema kuwa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) inapaswa kufanya juhudi za kuhimiza utulivu na ustawi wa kikanda, na wakati huo huo kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya pamoja ya dunia.
Waziri Mkuu Li Qiang alisema hayo kwenye Mkutano wa 25 wa Baraza la Wakuu wa Serikali (Waziri Mkuu) wa Nchi Wanachama wa SCO uliofanyika Dushanbe, mji mkuu wa Tajikistan.
Li Qiang alisema kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa SCO, na mkutano wa kilele uliofanyika Bishkek mwezi Septemba ulipata mafanikio muhimu yaliyoongeza nguvu mpya kwa ajili ya kuhimiza amani na maendeleo.
Aliongeza kuwa, wakati huohuo, mambo yanayoleta hali zisizo tulia na zisizo na uhakika duniani yanaendelea kuongezeka.
Alisema kuwa katika mkutano wa kilele wa Bishkek, Rais Xi Jinping wa China alisema kuwa katika njia panda inayohusiana na mustakabali wa binadamu, SCO inapaswa kubeba majukumu ya kihistoria na kufanya kazi kwa hiari katika kuongoza mchakato wa historia.
Li alisema kuwa ili kufikia lengo hilo, pande zote zinahitaji kufikia maoni mengi ya pamoja kwenye kanuni za kimsingi kuhusu matarajio, mawazo na fikra, pamoja na mbinu za kivitendo kuhusu uendeshaji na utekelezaji.
Li Qiang alitoa wito wa kuwa na uelewa na mawazo juu ya mambo ya dunia nzima, na kuwa na nia ya kubeba wajibu mkubwa kwa dunia, akieleza kuwa SCO inapaswa kuendelea kufuata “Moyo wa Shanghai.”
Baada ya mkutano, Waziri Mkuu Li Qiang pamoja na viongozi wengine wa nchi wanachama wa SCO walitia saini ya kutoa taarifa ya pamoja, kupitisha nyaraka za ushirikiano zinazohusu biashara na uwekezaji, viwanda na mafungamano ya mawasiliano, pamoja na azimio kuhusu maendeleo ya SCO.

Tarehe 20 Oktoba 2026, Waziri Mkuu wa Baraza la Serikali la China Li Qiang akihudhuria kwenye Mkutano wa 25 wa Baraza la Wakuu wa Serikali (Waziri Mkuu) wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai huko Dushanbe, Tajikistan. (Xinhua/Huang Jingwen)

Meli hospitali ya jeshi la majini la China yawasili Cote d'Ivoire kutekeleza jukumu la matibabu

Tamasha la 19 la Utamaduni na Utalii la A-Ma lafunguliwa Macao, China

Utandazaji wa reli waanza kwenye reli ya mwendo-kasi ya Nantong-Ningbo mkoani Jiangsu, China

Mabaki ya vivutio vya kihistoria vya Safari Ndefu mkoani Sichuan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma