Meli hospitali ya jeshi la majini la China yawasili Cote d'Ivoire kutekeleza jukumu la matibabu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 16, 2026

Vikosi vya gwaride la heshima vya nchini Cote d'Ivoire vikiikaribisha meli ya hospitali ya ‘Baraka’ ya Jeshi la Majini la Ukombozi wa Umma la China, wakati ikiwasili Abidjan, Cote d'Ivoire, tarehe 14 Oktoba 2026. (Picha na Yvan Sonh/Xinhua)

Vikosi vya gwaride la heshima vya nchini Cote d'Ivoire vikiikaribisha meli ya hospitali ya "Auspicious Ark" ya Jeshi la Majini la Ukombozi wa Umma la China, wakati ikiwasili Abidjan, Cote d'Ivoire, tarehe 14 Oktoba 2026. (Picha na Yvan Sonh/Xinhua)

ABIDJAN – Meli ya hospitali ya "Auspicious Ark" ya Jeshi la Majini la Ukombozi wa Umma la China (PLA), imewasili Abidjan, mji mkuu wa kiuchumi wa Cote d'Ivoire, Jumatano wiki hii kuanza ziara yake ya kirafiki na kutoa huduma za matibabu. Hii ni ziara ya kwanza ya meli hiyo ya hospitali ya jeshi la majini la China katika nchi hiyo.

Meli hiyo inayotekeleza "Jukumu la Masikilizano 2026" ilitia nanga Abidjan majira ya saa 4:00 asubuhi kwa saa za huko (1000 GMT).

Maofisa wa jeshi na serikali ya Cote d'Ivoire, Balozi wa China nchini Cote d'Ivoire, ofisa wa jeshi na wafanyakazi wa ubalozi wa China nchini humo pamoja na wajumbe wa wakazi Wachina na kampuni za China huko, waliikaribisha meli hiyo bandarini.

Wakiwa kwenye meli, askari wa jeshi la majini la China na wafanyakazi wa kiraia walisimama kirasmi na kuupungia mikono umati wa watu waliokuwa wakiwakaribisha bandarini.

Kwenye hafla hiyo ya kuwakaribisha, wakazi wenyeji walibeba mabango na kupeperusha bendera za China na Cote d'Ivoire ili kuikaribisha meli hiyo ya hospitali ya jeshi la majini la China. Baada ya hafla hiyo, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Majini la Cote d'Ivoire alipanda kwenye meli hiyo na kutembelea ndani ya meli.

Wakati wa ziara hiyo ya siku saba, meli hiyo itatoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa huko ndani ya meli, wakati huohuo madaktari watatembelea Hospitali ya Jeshi ya Abidjan na chuo kikuu kimoja nchini humo, ambapo watabadilishana uzoefu wa matibabu na kutoa huduma za matibabu.

Ujumbe huo pia utaandaa tafrija ndani ya meli hiyo ili kuongeza urafiki na kuaminiana na upande wa Cote d'Ivoire.

China na Cote d'Ivoire zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia mwezi Machi mwaka 1983 na kuanzisha rasmi ushirikiano wa kimkakati Septemba 2024.

Meli ya hospitali ya ‘Baraka’ ya  Jeshi la Majini  la China, ikiwasili Abidjan, Cote d'Ivoire, tarehe 14 Oktoba 2026. (Picha na Yvan Sonh/Xinhua)

Meli ya hospitali ya "Auspicious Ark" ya Jeshi la Majini la China, ikiwasili Abidjan, Cote d'Ivoire, tarehe 14 Oktoba 2026. (Picha na Yvan Sonh/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha