Wizara ya Biashara: China inapinga kithabiti vikwazo vya Marekani dhidi ya kampuni za China za AI

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 21, 2026

Wizara ya Biashara ya China jana Jumanne ilitoa malalamiko makali na kupinga kwa uthabiti hatua mpya ya Marekani ya kuamuru mashirika ya serikali yake kuu ya kiraia kuacha kutumia bidhaa na huduma za AI za kampuni za China.

Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China alisema kuwa China inashikilia kuweka mkazo na kutilia maanani sawa kuhusu maendeleo na usalama, ili kuhakikisha teknolojia ya AI inaweza kudumisha hali ya usalama, inaweza kudhibitiwa na kutegemewa.

Kampuni za China ya AI siku zote zinajikita katika kutoa huduma salama zinazotegemeka kwa watumiaji wa dunia nzima, wakati huo huo zinafuata sheria za nchi ziliko, na hivyo zimetambuliwa na nchi nyingi duniani.

Msemaji alisisitiza kuwa upande wa Marekani, kwa kisingizio cha kile kinachoitwa "usalama wa nchi", umechukua hatua za vizuizi za kibaguzi dhidi ya kampuni za China za AI, hii ni mbinu yake ya muda mrefu ya kutafsiri kupita kiasi dhana ya usalama wa nchi na kutumia ovyo njia za kiutawala kwa kushinikiza kampuni za China.

Msemaji alisema kuwa hali hii imedhuru vibaya haki na maslahi halali ya kampuni za China, kuharibu mazingira ya soko ya kufanya ushindani kwa usawa, na kuvuruga ushirikiano wa kawaida wa kibiashara kati ya China na Marekani katika nyanja ya AI.

Upande wa China unataka upande wa Marekani urekebishe mara moja hatua hiyo ya makosa, kuacha kushinikiza ovyoovyo kampuni za China, na kuondoa hatua hizo za vizuizi za kibaguzi. China inatumai upande wa Marekani utatekeleza kihalisi maoni muhimu ya pamoja yaliyofikiwa na wakuu wa nchi mbili na kutumia vizuri mfumo wa mazungumzo kati ya China na Marekani kuhusu AI.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha