Li Qiang ahudhuria mkutano wa 31 wa kawaida kati ya mawaziri wakuu wa China na Russia

(CRI Online) Oktoba 22, 2026

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang usiku wa Oktoba 20 aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Pulkovo mjini Saint Petersburg akahudhuria mkutano wa 31 wa kawaida kati ya mawaziri wakuu wa China na Russia.

Li amesema huu ni mwaka wa 30 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Russia na mwaka wa 25 tangu kusainiwa kwa Mkataba wa Ushirikiano na Ujirani Mwema kati ya nchi hizo mbili. Amesema uhusiano kati ya China na Russia umeweka mfano wa kuigwa wa uhusiano kati ya nchi kubwa wenye ujirani mwema wa kudumu, uratibu kamili wa kimkakati na ushirikiano wa kunufaishana.

Li ameongeza kuwa China inapenda kufanya juhudi endelevu na Russia, kuimarisha uhusiano wa nchi mbili na kuhimiza ushirikiano wa pande mbili kuzaa matunda mapya, ili kunufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili, na pia kuingiza utulivu na uhakika kwenye amani na maendeleo ya dunia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha