Mgonjwa wa kwanza wa Ebola athibitishwa nchini Nigeria, Afrika CDC yataka Dunia nzima kuimarisha mshikamano na kudhibiti maambukizi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 22, 2026

Tarehe 18 Oktoba 2026, mhudumu wa afya akimpima mgonjwa aliyeambukizwa Ebola katika kituo cha matibabu ya Ebola huko Bunia, mji mjii wa Mkoa wa Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Cong. (Xinhua)

Tarehe 18 Oktoba 2026, mhudumu wa afya akimpima mgonjwa aliyeambukizwa Ebola katika kituo cha matibabu ya Ebola huko Bunia, mji mjii wa Mkoa wa Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Cong. (Xinhua)

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) kimetoa wito wa kuimarisha mshikamano wa dunia nzima na uungaji mkono wa kimataifa ili kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi vya Ebola vya aina ya Bundibugyo yanayoenea kwa kasi.

Siku ya Jumanne wiki hii, serikali ya Nigeria ikifanya vipimo kwenye maabara imethibitisha kuwa mgonjwa wa kwanza aliyeambukizwa Ebola amegunduliwa Abuja, mji mkuu wa nchi hiyo. Hii ilifuatiwa na wito wa dharura kutoka kwa serikali.

Ali Pate, Waziri wa Afya na Uratibu wa Huduma za Jamii alisema, mwanamke mmoja aliyewasili Nigeria hivi karibuni kwa ndege kutoka Uganda amewekwa kwenye karantini na anapatiwa matibabu, na mamlaka zinafanya juhudi za kuzuia virusi hivyo vinavyosababisha homa ya kutokwa na damu visienee katika maeneo ya wakazi.

Nchi hii ya Afrika Magharibi imekuwa nchi ya nne barani Afrika kugunduliwa kwa mgonjwa wa Ebola aliyethibitishwa. Kabla ya hayo virusi hivi hatari vimeathiri nchi tatu nyingine za Afrika — Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Uganda na Kenya.

“Kabisa hatutaweza kuacha mlipuko huu uenee hadi nchi nyingi zaidi, wala kuuacha uendelee kuwepo kwa mwaka mmoja tena,” Jean Kaseya, Mkurugenzi Mkuu wa Africa CDC, alionya katika taarifa aliyoitoa Jumanne jioni. Alisema huu maambuziki ya virusi vya Ebola ya mara hii sasa yamekuwa maambukizi yanayoenea kwa mapana zaidi kijiografia katika historia yake.

Alisema Africa CDC imeanza kuhamasisha nguvu za pande mbalimbali kusaidia Nigeria, wakati huo huo imeongeza uitikio wake kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Kenya, na kukaa kwa macho zaidi juu ya hali ya nchini Uganda.

“Natoa wito wa dharura kwa jumuiya ya kimataifa: fanya vitendo halisi mara moja. Tunahitaji mitaji inayoweza kufika kwa wakati na kwa unyumbufu, pamoja na dawa na vifaa vya matibabu, vifaa vya upimaji, wafanyakazi waliopata mafunzo wenye uwezo wa kukabiliana na hali ya dharura, na kufanya ufuatiliaji wenye nguvu zaidi kwa maeneo ya wakazi,” alisema Kaseya.

Tarehe 18 Oktoba 2026, wahudumu wa afya wakifanya kazi ya kusafisha kwa dawa ya kuua bakteria katika kituo cha matibabu ya Ebola huko Bunia, mji mkuu wa Mkoa wa Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. (Xinhua)

Tarehe 18 Oktoba 2026, wahudumu wa afya wakifanya kazi ya kusafisha kwa dawa ya kuua viini katika kituo cha matibabu ya Ebola huko Bunia, mji mkuu wa Mkoa wa Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. (Xinhua)

Tarehe 18 Oktoba 2026, mhudumu wa afya akifuatilia hali ya mtoto aliyeambukizwa virusi vya Ebola katika kituo cha matibabu ya Ebola huko Bunia, mji mkuu wa Mkoa wa Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. (Xinhua)

Tarehe 18 Oktoba 2026, mhudumu wa afya akifuatilia hali ya mtoto aliyeambukizwa virusi vya Ebola katika kituo cha matibabu ya Ebola huko Bunia, mji mkuu wa Mkoa wa Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. (Xinhua)

Tarehe 18 Oktoba 2026, mhudumu wa afya akisafisha mikono yake kwa dawa ya kuua bakteria  katika kituo cha matibabu ya Ebola huko Bunia, mji mkuu wa Mkoa wa Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Cong. (Xinhua)

Tarehe 18 Oktoba 2026, mhudumu wa afya akisafisha mikono yake kwa dawa ya kuua viini katika kituo cha matibabu ya Ebola huko Bunia, mji mkuu wa Mkoa wa Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Cong. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha