Lugha Nyingine
Rais wa China ahutubia Mkutano wa Kuadhimisha Miaka 90 ya Ushindi wa Safari Ndefu ya Jeshi Jekundu la China
Rais wa China Xi Jinping amehudhuria na kuhutubia Mkutano wa Kuadhimisha Miaka 90 ya Ushindi wa Safari Ndefu ya Jeshi Jekundu la China uliofanyika jana Oktoba 22 hapa Beijing.
Katika hotuba yake, rais Xi amesema, Safari Ndefu ambalo ni tukio kubwa la kimapinduzi lina umuhimu mkubwa katika historia ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), nchi na jeshi, na limetoa mchango mkubwa katika mchakato wa kuelekea ustawi mpya wa taifa la China.
Amesema tukio hilo la kishujaa litawekwa daima katika mnara wa kumbukumu ya mapinduzi ya China, na pia kukumbukwa milele mioyoni mwa wananchi.
Pia amesisitiza kuwa, Chama, wanajeshi wote na watu wa makabila yote nchini lazima waungane kwa karibu zaidi na Kamati Kuu ya CPC, waendeleze kwa nguvu moyo wa Safari Ndefu, waendelee kujitahidi na kusonga mbele, ili kuhimiza kazi kubwa iliyoanzishwa na watangulizi wa kimapinduzi, nakutimiza mafanikio mapya katika Safari Ndefu mpya.

Meli hospitali ya jeshi la majini la China yawasili Cote d'Ivoire kutekeleza jukumu la matibabu

Tamasha la 19 la Utamaduni na Utalii la A-Ma lafunguliwa Macao, China

Utandazaji wa reli waanza kwenye reli ya mwendo-kasi ya Nantong-Ningbo mkoani Jiangsu, China

Mabaki ya vivutio vya kihistoria vya Safari Ndefu mkoani Sichuan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma