Lugha Nyingine
Mada ya "China Haul" inaonyesha mvuto unaozidi kuongezeka wa kununua nchini China

Tarehe 30 Aprili 2026, watalii wa kigeni wakichagua vitu katika duka kuu la Huawei jijini Beijing. (Xinhua/Ju Huanzong)
Wizara ya Biashara ya China imesema, mada inayovuma ya "China Haul" kwenye mitandao ya kijamii ya kimataifa inaonesha watu wanazidi kutambua na kupenda "manunuzi nchini China".
Mkurugenzi wa Ofisi kuu ya Uendeshaji wa Soko na Ukuzaji wa Matumizi katika Wizara ya Biashara ya China Yang Mu amesema, hali ya wageni kueleza maoni yao na furaha zao za kununua vitu nchini China kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii ya kimataifa pia imeonesha ufunguaji mlango wa China wa kufuata vigezo vya juu, na mvuto wa utamaduni wa kijadi wa China.
Katika mkutano na waandishi wa habari wa jana Alhamisi, Yang alipotoa maelezo kuhusu maendeleo yenye hali ya ustawi katika matumizi ya wageni wanaoingia nchini China alisema kwamba aina za bidhaa wanazozipendelea watumizi kutoka nchi za nje zinapanua kutoka bidhaa za jadi kama chai na hariri, hadi bidhaa za kiteknolojia, vitu vya kusaidia afya vya China, vipodozi na vitu vya kuchezea vya kufuata wimbi.
Yang amesema, kununua vitu kumekuwa madhumuni muhimu ya kuja China kusafiri kwa watalii wa nchi za nje, mbali na kufanya utalii katika miji mikubwa mbalimbali, watalii wa kigeni sasa pia wanatembelea maeneo mengi zaidi nchini China.
Katika robo ya tatu ya mwaka 2026, China iliendelea kuvutia watalii wengi zaidi kutoka nchi mbalimbali, huku idadi ya walioingia kupitia msamaha wa visa ikiongezeka kwa asilimia 24.1 kuliko mwaka uliopita, na safari za watalii wa kigeni zilikaribia milioni tisa.
Kwenye msingi wa mpango wa msamaha wa visa wa China unaoendelea kupanuliwa, mfululizo wa sera na hatua pia zimetolewa na kuwapa watalii wa kigeni urahisi zaidi wa kununua vitu nchini China. Sera na hatua hizo ni pamoja na kuboreshwa kwa sera ya urejeshaji wa kodi kwa watalii kabla ya kuondoka nchini China.
Takwimu rasmi zinaonyesha kwamba hivi sasa nchini China kumekuwepo zaidi ya maduka 18,000 ya urejeshaji wa kodi, hii imefikia ongezeko la asilimia 400 kuliko lile la mwisho wa mwaka 2024.

Meli hospitali ya jeshi la majini la China yawasili Cote d'Ivoire kutekeleza jukumu la matibabu

Tamasha la 19 la Utamaduni na Utalii la A-Ma lafunguliwa Macao, China

Utandazaji wa reli waanza kwenye reli ya mwendo-kasi ya Nantong-Ningbo mkoani Jiangsu, China

Mabaki ya vivutio vya kihistoria vya Safari Ndefu mkoani Sichuan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma