Pale ujasiri unapoishia, ustadi unafikia kilele — njia ya kujiendeleza ya mwokoaji anayetumia kamba

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 23, 2026

Tarehe 25 Machi 2022, Jiang Shengqiang akifanya kazi ya uokoaji katika eneo la ajali ya ndege ya China Eastern namba MU5735 katika Wilaya ya Tengxian, Mkoa unaojiendeshax wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi. (Xinhua)

Tarehe 25 Machi 2022, Jiang Shengqiang akifanya kazi ya uokoaji katika eneo la ajali ya ndege ya China Eastern namba MU5735 katika Wilaya ya Tengxian, Mkoa unaojiendeshax wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi. (Xinhua)

Katika sehemu ya ndani kabisa ya pango lenye umbo la S katika mji wa Liuzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi kusini mwa China, Jiang Shengqiang na timu yake walitambaa kwa kupita njia nyembamba iliyokuwa na nafasi ya kuwezesha mtu mmoja tu kupita. Katika sehemu ya kina cha takriban mita 80 chini ya ardhi, mchunguzaji mmoja wa mapango alishindwa kufanya chochote kwa sababu ya mifupa mingi kuvunjika. Waokoaji hao walitoboa miamba kufungua njia, wakafunga kamba katika maeneo kadhaa, na wakamwekea mwanamume aliyejeruhiwa jaketi la wazima moto chini yake ili kumwepusha madhara ya ardhi yenye miamba, kisha wakamwinua kuelekea mlangoni wa pango.

Mnamo Februari 2025, saa 15 baada ya operesheni ya uokoaji kuanza, mwanamume huyo aliokolewa salama na kufika kwenye ardhi.

Kwa Jiang, kiongozi wa timu ya uokoaji wa milimani ya Idara ya Wazima Moto na Uokoaji ya mji wa Liuzhou, operesheni hii ilitumia ujuzi ambao alifanya mazoezi kwa bidii kwa miaka mingi. Na juhudi zake za kujifunza ujuzi huo zilianza katika operesheni moja ya uokoaji mwaka 2008.

Mwaka huo, msichana mmoja alianguka kutoka mlima na kwamwa kwenye mti mwenye urefu wa zaidi ya mita 80 chini ya mlima, Jiang pamoja na wenzake waliitwa kwa dharura. Wakati huo, wazima moto wa timu hiyo bado hawajajua sana kuhusu ujuzi wa kitaalamu wa uokoaji wa sehemu za milimani. Hatimaye walimpata msichana huyo na kumwokoa, lakini mchakato mzima ulichukua saa 10.

"Niliona wazazi wake wakiwa na wasiwasi mkubwa, na nilijisikia hatia," Jiang anakumbuka. "Wakati huo, kilichobaki nasi ni ujasiri tu. Nilijua tunahitaji ujuzi unaolingana na hali hiyo."

Alipata kwa mara ya kwanza mafunzo kikamilifu mnamo mwaka 2016, ambapo alihudhuria darasa la mafunzo ya uokoaji wa majini na milimani, na kufundishwa ujuzi wa kitaalamu wa utumiaji wa kamba. Alijikita kwa nguvu zote katika kubobea ujuzi huo.

Katika miaka mingi iliyopita, maelfu ya mita za kamba zilichakaa katika mazoezi yake. Katika muda wa zaidi ya miaka miwili tu, Jiang alipata vizuri ujuzi wa uokoaji kwa kutumia kamba moja au kamba mbili. Hadi mwaka 2019, alikuwa tayari ameanza kuwafundisha wakoaji wengine.

Mazingira ya kazi pembezoni mwake pia yalikuwa yakibadilika.

Baada ya kikosi cha wazima moto na uokoaji cha China kupangwa upya mwaka 2018, majukumu yake yalipanua kutoka kuzima moto hadi nyanja pana zaidi za uokoaji wa dharura. Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Usimamizi wa Dharura, hadi Julai 2021, China ilikuwa imeunda timu 179 za kitaalamu za uokoaji wa sehemu za milimani zenye wafanyakazi zaidi ya 3,500, ambapo wakoaji 752 walikuwa na uwezo wa uokoaji kwa kutumia kamba.

Jiang aliwafundisha wenzake wote 20 wa timu yake. Timu hiyo iliandaa zaidi ya taratibu 10 za uokoaji, na kuboresha mfumo wa kuwaokoa watu waliokwamwa katika mafuriko ya maji, ikipunguza idadi ya wafanyakazi wanaohitajika kutoka 8 hadi 5. Mapendekezo matano aliyotoa Jiang baadaye yalijumuishwa katika mtaala wa mafunzo ya uokoaji ya kitaifa.

Jiang amefanya kazi katika idara ya wazima moto na uokoaji kwa zaidi ya miaka 19, na ameshiriki katika operesheni zaidi ya 4,000 za uokoaji wa dharura na kusaidia kuwaokoa zaidi ya watu 300.

Tarehe 8 Februari 2025, wanachama wa timu ya uokoaji wa sehemu za milimani ya idara ya wazima moto na uokoaji ya mji wa Liuzhou wakifanya uokoaji katika pango moja huko Liuzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi. (Xinhua)

Tarehe 8 Februari 2025, wanachama wa timu ya uokoaji wa sehemu za milimani ya idara ya wazima moto na uokoaji ya mji wa Liuzhou wakifanya uokoaji katika pango moja huko Liuzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi. (Xinhua)

Tarehe 20 Juni 2026, Jiang Shengqiang (katikati, nyuma) akiwaongoza wenzake wa timu katika mafunzo ya uokoaji kwa kutumia kamba katika kituo cha mafunzo huko Liuzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi. (Xinhua/Yang Chi)

Tarehe 20 Juni 2026, Jiang Shengqiang (katikati, nyuma) akiwaongoza wenzake wa timu katika mafunzo ya uokoaji kwa kutumia kamba katika kituo cha mafunzo huko Liuzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi. (Xinhua/Yang Chi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha