Mitambo ya kampuni ya China yasaidia juhudi za uokoaji kwenye jengo lililoanguka Nairobi

(CRI Online) Oktoba 26, 2026

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Kampuni ya Mashine za Ujenzi ya China (XCMG) imeshiriki katika juhudi za uokoaji na kusaidia kuokoa watu wawili baada ya kuanguka kwa jengo la ghorofa mjini Nairobi.

Ofisa anayesimamia raslimali watu katika eneo la Nairobi Kaskazini, Bw. William Sifuna Watitwa, amethibitisha kuwa kampuni hiyo ilitoa mashine ya kuchimba na kreni yenye uwezo wa kubeba tani 25 ili kusaidia katika juhudi za utafutaji.

Kreni hiyo iliwawezesha wahudumu wa dharura kufanya kazi hiyo kutoka juu, kwa kuinua kifusi ili kupunguza uzito na kurahisisha ufikiaji wa watu ambao huenda bado wako hai kwenye kifusi.

Maofisa wa serikali wamesema watu watano bado hawajapatikana, na wengine wanne wako hospitali kupata matibabu. Msimamizi katika ofisi ya XCMG nchini Kenya Bw. Fredrick Nyasani, amesema kampuni hiyo ilipeleka mitambo hiyo mara tu baada ya kupata taarifa kuhusu kuanguka kwa jengo hilo.

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha